Thursday, September 20, 2012

RONAN KEATING APATA MPENZI KIPYA























Ronan Patrick John Keating alias Ronan Keating






















Ronan Keating akiwa na mpenzi wake mpya.  


Ronan Patrick John Keating alias Ronan Keating mwanamuziki maarufu toka Ireland na pia mtunzi wa nyimbo ambaye ameshatamba na single zake kama “This I Promise You” na “When You Say Nothing” kwa sasa ameanza kupata furaha ya mapenzi baada ya kupata mpenzi mpya.

Mpenzi wake mpya huyo anajulikana kama Storm Uechtritz, Keating na Storm walianza mahusiano mara baada ya kutengana na mpenzi wake wa awali.

Ronan Keating ambaye alishawahi kuwa mmoja wa wanamuziki wa kundi la Boyzone amepata mpenzi  mwingine wakati akiwa katika X-Factor huko Australia ambako alikuwa ni muandaaji. Ronan mwenye miaka 35 sasa ndoa yake ya miaka 14 na Yvonne iliisha rasmi Aprili mwaka huu kutokana na kashfa iliyomkuta kwa kufanya mapenzi na dansa wake.

mwanamuziki maarufu toka Ireland na pia mtunzi wa nyimbo ambaye ameshatamba na single zake kama “This I Promise You” na “When You Say Nothing” kwa sasa ameanza kupata furaha ya mapenzi baada ya kupata mpenzi mpya. Mpenzi wake mpya huyo anajulikana kama Storm Uechtritz, Keating na Storm walianza mahusiano mara baada ya kutengana na mpenzi wake wa awali. Ronan Keating ambaye alishawahi kuwa mmoja wa wanamuziki wa kundi la Boyzone amepata mpenzi mwingine wakati akiwa katika X-Factor huko Australia ambako alikuwa ni muandaaji. Ronan mwenye miaka 35 sasa ndoa yake ya miaka 14 na Yvonne iliisha rasmi Aprili mwaka huu kutokana na kashfa iliyomkuta kwa kufanya mapenzi na dansa wake.

Diamond Platnumz: Nataka kutengenza ajira kwa vijana wenzangu MSANII wa Kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema amedhamiria kutoa ajira kwa vijana wengi wa kitanzania kupitia muziki huku pia akileta mapinduzi katika sekta hiyo nchini. Diamond ambaye ni msanii ghali zaidi kwa sasa Tanzania, amesema kuna watu wengi wenye vipaji ambao wako mtaani au wako katika sekta nyingine lakini hawajui wafanyeje ili kufikia ndoto zao jambo ambalo linahitaji watu wengine wawasaidie kuwafikisha pale wanapotaka. “Kuna tatizo ambalo lipo katika mambo ya mitindo, muziki. Watu wengi wanachukulia kama uhuni, wengi wanaona kama kuuza sura, yaani mtu aonekane kwenye video ili apate umaarufu, tunatakiwa kubadilisha mawazo haya, Ulaya hata hapo Afrika Kusini wanaonekana kwenye video wanalipwa. “Mimi nitawalipa wote watakaonekana kwenye video yangu, tutakapofanya usaili kesho wale watakaochanguliwa watalipwa, lakini pia hii inaweza kuwa ni kufunguliwa milango kwenye sekta nyingine, wapo wanaoweza kuonekana wanafaa kwenye matangazo ya biashara, hawa watapata kampuni ambazo zinaweza kuwatumia. “Katika majaji watakuwepo Raqey Mohammed wa I-View Studios, hawa wanafanya kazi nyingi za matangazo, movie, atakuwepo pia Ally Rehmtulah huyu ni mbunifu anaweza kumuona mtu na akasema huyu anafaa kwa sekta yake, Sammy Cool ni densa na mwalimu hata Missie Popular yeye ni mwandishi na mwanamitindo wanajua wapi kwa kuwafikisha watu wengine’ alisema. Msanii huyo alisema mafanikio aliyo nayo ya kumiliki nyumba, magari na kujulikana kwake yametokana na muziki, hivyo ana uhakika wapo watu wengine pia kupitia yeye na wanamuziki wengine kama yeye wanaweza kufaidika na kufikia mafanikio kama aliyoyapata. Diamond alisema usaili huo unafanyika kesho pale nyumbani Lounge kuanzia saa tano asubuhi. Hii ni mara ya kwanza kwa msanii wa nchini kufanya usaili kwa ajili ya watu watakaonekana kwenye video yake. Diamond pia ndiye msanii wa kwanza wa muziki wa kizazi kipya kuandaa shoo yake mwenyewe na watu kulipa kiingilio cha sh 50,000. Diamond alifanya hivyo kwenye onyesho alilolipa jina la Diamond are Forever pale Mlimani City, Dar es Salaam. Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Majaji usaili wa video ya Diamond watangazwa MSANII wa Kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ataongoza jopo la majaji wengine wanne kwa ajili ya kupata wasichana na wavulana watakaoshiriki kwenye video yake mpya. Usaili wa watu hao utafanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge, mjini Dar es Salaam ambao wote watakaochaguliwa kuonekana kwenye video hiyo itakayorekodiwa na kampuni ya I-View Studios watalipwa. Katika orodha hiyo, yupo mbunifu wa mitindo wa kimataifa, Ally Rehmtullah ambaye hivi karibuni alizundua mavazi yake mapya katika hoteli ya Serena, yupo pia Raqey Mohamed ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya I-View Studios,pia Creative Director, Sammy Cool ambaye ni mwalimu wa dansi na blogger maarufu Missie Popular. Akizungumza mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema majaji hao wamechaguliwa kutokana na kuhusika kwao na shughuli za sanaa kila siku. “Diamond ndiye mwenye video na ni mwanamuziki, Raqey ndiye atakayerekodi video, lazima ajue watu ambao ana wataka kwenye hiyo video, ameshafanya kazi kama hizi mara nyingi, ni mpiga picha wa kimataifa, Sammy Cool ni densa maarufu na mwalimu ambaye amewafundisha watu wengi katika ulimwengu wa kucheza nchini, wengi watakuwa wakimfahamu tangu enzi za Bombeso, THT na mashindano mbalimbali ya urembo, amekuwa pia akitoa ushauri nasaha. “Kwa upande wa Ally ni mbunifu wa mitindo wa kimataifa, ameshafanya kazi mpaka ulaya, ana uzoefu mkubwa kutokana na kazi zake kwa hiyo kuwepo kwake kutasaidia pia vipaji vingine kuonekana, Missie Popular yeye ni mwandishi, mwanamitindo kwa hiyo kama mtu wa habari ana mchango wake katika kuibua vipaji pia,” amesema. Mwendapole amesema usaili huo utaanza saa tano kamili asubuhi na kwamba baada ya usahili huo wale watakaochaguliwa watafahamishwa mazoezi yatakuwa wapi na baada ya hapo kazi ya kurekodi video hiyo kuanza. Video hiyo ambayo wote watakaochaguliwa kuonekana watalipwa, itarekodiwa maeneo mbalimbali nchini pamoja na sehemu nyingine nje ya bara la Afrika ili kuipa ladha tofauti. Kampuni ya I-View ndio imeshinda mchakato wa kurekodi video hiyo. Tayari kampuni hiyo imeweza kutengeneza video kadhaa za kiwango cha kimataifa ikiwemo Kwasakwasa Tazneem, Utanikumbuka ya Suma Lee pamoja na matangazo mbalimbali ya biashara. I-View pia ndiyo inatengeneza kava za wasanii mbalimbali Bongo Movie ambao wanafanya kazi na Steps Entertainment. Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx RONAN KEATING APATA MPENZI KIPYA Ronan Keating akiwa na mpenzi wake mpya. Ronan Patrick John Keating alias Ronan Keating mwanamuziki maarufu toka Ireland na pia mtunzi wa nyimbo ambaye ameshatamba na single zake kama “This I Promise You” na “When You Say Nothing” kwa sasa ameanza kupata furaha ya mapenzi baada ya kupata mpenzi mpya. Mpenzi wake mpya huyo anajulikana kama Storm Uechtritz, Keating na Storm walianza mahusiano mara baada ya kutengana na mpenzi wake wa awali. Ronan Keating ambaye alishawahi kuwa mmoja wa wanamuziki wa kundi la Boyzone amepata mpenzi mwingine wakati akiwa katika X-Factor huko Australia ambako alikuwa ni muandaaji. Ronan mwenye miaka 35 sasa ndoa yake ya miaka 14 na Yvonne iliisha rasmi Aprili mwaka huu kutokana na kashfa iliyomkuta kwa kufanya mapenzi na dansa wake. Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx EXCLUSIVE : SHAKIRA MJAMZITO Shakira. Shakira akiwa na Gerard Pique. Mwimbaji kutoka Colombia kwa jina la Shakira ni mjamzito na anatarajia kupata mtoto wake huyo wa kwanza. The Hips don’t Lie singer mwenye umri wa miaka 35 amethibitisha kuwa ana mimba na wanatarajia kupata mtoto wa pamoja na Spanish footballer Gerard Pique anayeichezea club ya Barcelona. Na zaidi Shakira ameamua kupunguza ratiba zake za kazi kuanzia week ijayo. Shakira amethibitisha kuwa mjamzito baada ya kuandika kwenye tovuti yake kwa kuwaambia mashabiki zake kama hivi:”As some of you may know, Gerard and I are very happy awaiting the arrival of our first baby. ‘At this time we have decided to give priority to this unique moment in our lives and postpone all the promotional activities planned over the next few days.” Mwimbaji huyu alikuwa anatarajiwa kuperform kwenye tamashsa la iHeartRadio Music Festival at the MGM Grand Hotel and Casino weekend hii huko Las Vegas, but had now cancelled her appearance. Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx NAS NA LAURYN HILL WATANGAZA TOUR YAO YA “LIFE IS GOOD/BLACK RAGE” Nas & Lauryn Hill wakiwa kwa stage. Hip-hop history is about to be made. Nas na Lauryn Hill wameamua kuungana na na kushirikiana kwenye ziara itayokwenda kwa jina la “Life Is Good/Black Rage”. Tour hii imeunganisha majina ya album mpya ya Nas kwa jina la “Life Is Good” na “Black Rage,” ambayo ni single mpya ya mwanadada Lauryn Hill ambayo inaelezea maswala mazima ya unyanyasaji na ubaguzi wa rangi ambapo anaamini kupitia nyimbo hiyo mambo hayo yatashughulikiwa na kutatuliwa. Kuhususiana na tour hii Nas anafunguka kwa kusema:“This is history. Better late than never. Life is good!”. Na kuhusu swala zima la Tickets zitaanza kuuzwa ijumaa ya kesho, ila kwa mauzo ya awali kwenye masoko tickets zimeanza kuuzwa alhamisi ya leo. Hii ndio Ratiba nzima na tarehe za “Life Is Good/Black Rage” Tour: Oct. 6 – Columbia, MD – Merriweather Post Pavilion (NAS ONLY) Oct. 20 – Phoenix, AZ – Arizona State Fairgrounds (NAS ONLY) Oct. 26 – Asheville, NC – MOOG Festival (NAS ONLY) Oct. 27 – Nashville, TN – Riverfront Park (NAS ONLY) Oct. 28 – New Orleans, LA – Voodoo Festival (NAS ONLY) Oct. 29 – Dallas, TX – Palladium Ballroom Oct. 31 – Houston, TX – Bayou Music Center Nov. 2 – Atlanta, GA – Tabernacle Nov. 3 – Norfolk, VA – NorVa Theatre (NAS ONLY) Nov. 4 – Washington, DC – DAR Constitution Hall Nov. 7 – Philadelphia, PA – Electric Factory Nov. 9 – Rochester, NY – Main Street Armory(NAS ONLY) Nov. 11 – Boston, MA – House of Blues Nov. 14 – Chicago, IL – Congress Theatre Nov. 16 – Denver, CO – Fillmore Auditorium Nov. 17 – Magna, UT – Salt Air Nov. 19 – Oakland, CA – Fox Oakland Theater Dec. 31 – New York, NY – Radio City Music Hall (NAS ONLY). Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Wednesday, September 19, 2012

TID ALILIA FIESTA.....!!!


Khaleed Mohamed aka TID now ameamua kuwa kutoa ya Moyoni katika kila jambo linalomkera. Siku moja baada ya kukaririwa akizungumzia juu ya issue yake dhidi ya Ali Kiba, leo ‘MNYAMAAAAAA’amezungumzia juu ya suala lake la kutokuwepo katika list ya wasanii wanao-perform katika the biggest music concert in Tanzania Fiesta. Kupitia his official facebook account TID ameandika status inayosomeka kama ifuatavyo: “I wiSh I coUld maKe the Guy Who does the FieSta Listing be oN my SiDe some PeoplE are workin verY Hard to juSt makE me Look like Criminal so I can not be on List Lakini Mungu atanipa Better than Fiesta tho its Been 5 years am nt Part of It”. Kwa maana hiyo owner huyo wa Top Band analalamika kwamba ana kila sifa ya kuwa mmoja ya wasanii wanaopanda katika jukwaa la tamasha hilo linaloendelea hivi sasa, lakini kwa sababu tofauti watu wanaoshughulika na kupanga listi ya wasanii wamekuwa wakimpotezea Mnyama kwa takribani miaka mitano iliyopita pamoja na kuwa hit songs nyingi ndani ya kipindi hicho

I-View Studio kurekodi Video mpya ya Diamond Platnumz


KAMPUNI I-View Studios ya mjini Dar es Salaam imeshinda mchakato wa kurekodi video mpya ya msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambayo usaili wake utafanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge, Dar es Salaam.

Akizungumza mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema I-View imepata nafasi hiyo kutokana na kiwango kikubwa cha video kadhaa ilizofanya lakini pia vifaa ilivyo navyo na uwezo wa wafanyakazi wake.
“Siku zote kila mtu anaangalia kitu kizuri, Diamond ametaka kufanya mapinduzi katika tasnia ya muziki, lakini kufanya mapinduzi kunahusisha vitu vingi, tungo zake yeye kama msanii, studio anayorekodia watu watakaoshiriki kwenye video yake kampuni itakayorekodi video pia, lakini mwisho wa siku I-View chini ya Raqey Mohamed ndio imeshinda nafasi hiyo.

“Raqey anafahamika kwa kazi zake pamoja na kurekodi matangazo mbalimbali ya Televisheni, picha mnato lakini pia video za wasanii Taznim ya Kwasakwasa, Utanikumbuka ya Suma Lee ni baadhi ya kazi ambazo zinaonyesha uwezo alionao lakini pia Diamond na timu yake tumeweza kuona vifaa vipya na vya kisasa ambavyo Raqey anavyo kwa sasa na hakuna kwa Afrika Mashariki na Kati,” alisema.

Kwa upande wake Raqey ambaye ni Mkurugenzi wa I-View alisema anahitaji kuifanya kazi hiyo kuwa tofauti ili kusukuma mbele sekta ya mawasiliano na muziki kwa ujumla.
“Sisi kama I-View tunafurahi kufanya kazi na Diamond, ni msanii mzuri na mkubwa ambaye kazi zake zinaonekana, hatutamuangusha na mashabiki na wasanii wengine wasubirie kazi itakapotoka,” alisema.

I-View pia watashiriki katika mchakato wa kupata watu watakaonekana kwenye video hiyo ambayo ni kwa mara ya kwanza nchini kutafanywa usaili wa washiriki. Usaili huo utafanyika Jumamosi katika ukumbi wa Nyumbani Lounge ambao unamilikiwa na mwanamuziki Lady Jaydee. Majina ya majaji wataochuja yatanatarajiwa kutangazwa leo.

Friday, September 14, 2012

Diamond Platnumz kufanya usaili watakaonekana video yake mpya

MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul, anatarajia kufanya usaili kwa ajili ya watu watakaotumika katika kurekodi video ya wimbo wake mpya ambao utaachiwa hivi karibuni.


Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema mjini Dar es Salaam kuwa Diamond amefikia uamuzi huo katika kuhakikisha kazi zake zinafanyika katika kiwango cha kimataifa.


“Jumamosi ijayo tutafanya usaili wa watu ambao wataonekana kwenye video hiyo, hii ni mara ya kwanza kwa kitu kama hiki kufanyika nchini kwetu ingawa wenzetu Ulaya wamekuwa wanafanya hivyo na wanaonekana wanakuwa wanalipwa tofauti na video nyingi za wasanii wa hapa kwetu na hao watakaochaguliwa kwenye video hiyo watalipwa pia,” alisema.




Akizungumzia kuhusu video hiyo, Mwendapole alisema itarekodi ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha inakidhi matakwa ya soko ambalo msanii huyo analiangalia kwa sasa huku video hiyo ikifanya na kampuni bora kabisa Tanzania.



Kwa upande wake Diamond alisema lengo kubwa la kufanya hivyo ni kuleta mapinduzi katika sekta ya muziki nchini lakini pia kutengeneza ajira kwa ajili ya wasichana na wavulana ambao wako mitaani lakini wanapenda muziki.



Diamond ambaye alikuwa nchini Marekani wiki iliyopita anatarajiwa tena kwenda Marekani kwa ajili ya onyesho moja la muziki.



Msanii huyo alifanya mapinduzi katika medani ya muziki wa bongo baada ya kufanya onyesho lake alilolipa jina la Diamond’s are Forever pale Mlimani City ambapo katika shoo hiyo aliifanya mwenyewe na kiingilio kikiwa sh 50,000 jambo ambalo halijawahi kufanyika katika ulimwengu wa muziki nchini.

Diamond Platnumz kufanya usaili watakaonekana video yake mpya

MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul, anatarajia kufanya usaili kwa ajili ya watu watakaotumika katika kurekodi video ya wimbo wake mpya ambao utaachiwa hivi karibuni.


Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema mjini Dar es Salaam kuwa Diamond amefikia uamuzi huo katika kuhakikisha kazi zake zinafanyika katika kiwango cha kimataifa.


“Jumamosi ijayo tutafanya usaili wa watu ambao wataonekana kwenye video hiyo, hii ni mara ya kwanza kwa kitu kama hiki kufanyika nchini kwetu ingawa wenzetu Ulaya wamekuwa wanafanya hivyo na wanaonekana wanakuwa wanalipwa tofauti na video nyingi za wasanii wa hapa kwetu na hao watakaochaguliwa kwenye video hiyo watalipwa pia,” alisema.

Diamond Platnumz kufanya usaili watakaonekana video yake mpya

MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul, anatarajia kufanya usaili kwa ajili ya watu watakaotumika katika kurekodi video ya wimbo wake mpya ambao utaachiwa hivi karibuni.


Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema mjini Dar es Salaam kuwa Diamond amefikia uamuzi huo katika kuhakikisha kazi zake zinafanyika katika kiwango cha kimataifa.


“Jumamosi ijayo tutafanya usaili wa watu ambao wataonekana kwenye video hiyo, hii ni mara ya kwanza kwa kitu kama hiki kufanyika nchini kwetu ingawa wenzetu Ulaya wamekuwa wanafanya hivyo na wanaonekana wanakuwa wanalipwa tofauti na video nyingi za wasanii wa hapa kwetu na hao watakaochaguliwa kwenye video hiyo watalipwa pia,” alisema.