Monday, January 28, 2013

Updates: Mpaka sasa Lulu hajatimiza masharti ya dhamana, huenda akarejea Segerea



Kwa mujibu wa vyanzo hadi muda huu (saa nane) Lulu bado hajaachiwa mahakamani kwakuwa bado taratibu za dhamana yake hazijakamilishwa.

Ili atoke ni lazima taratibu na masharti yote yatimizwe na kisha kusaniniwa na Msajili wa Mahakama Kuu ambapo kama muda wa saa za kazi wa serikali ukiisha bila kukamiliswa Lulu atarejeshwa tena mahabusu, Segerea.

Kama leo asipoachiwa kutokana na hali hiyo kesho atapelekwa tena mahakamani hapo kwa ‘remove order’ na kisha kuachiwa.

Video: Chris Brown na Frank Ocean wazichapa studio

Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Chris Brown usiku wa kuamkia leo amezichapa kavu kavu na mwanamuziki mwenzie Frank Ocean.Vyanzo vilivyo karibu na Chris vimedai kuwa Chris anadai Ocean ndiye aliyeanzisha ugomvi.

Chris alikuwa kwenye studio ya Westlake ya jijini Los Angeles akisikiliza baadhi ya nyimbo za wasanii wake. Vyanzo vinasema wakati Chris anaondoka, Frank Ocean na washkaji zake wakaziba njia. Vyanzo vimesema Frank alisema “This is my studio, this is my parking spot.”

Kwenye Youtube kuna video hii ambayo ina maelezo yasemayo: THIS IS CHRIS BROWN SECURITY GUARD & FRANK OCEAN FIGHTING, CHRIS BROWN LEFT BECAUSE HIS HAND WAS CUT BAD. I STARTED RECORDING LATE.


Mtandao huo umesema Chris alienda kumpa mkono Frank na ndipo washkaji wa Frank walipomvamia Chris. Vyanzo vilivyo karibu na Chris Brown vimesema rafiki wa Chris aliruka mbele na kumpiga rafiki yake na Frank.Inadaiwa kuwa Frank alimfuata Chris na akasumwa na Chris na ndipo walipoanza kupigana.

Baadaye polisi waliwasili na hakuna anayetaka kufungua kesi.

Dr Cheni: Niko tayari kumtolea Lulu dhamana ya shilingi milioni 20



Muigizaji wa Bongo Movie Dr. Cheni amesema yeye ni miongoni mwa watu walio tayari kumdhamini muigizaji mwenzie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye leo hii mahakama kuu ya Tanzania imempa nafasi ya dhamana.

Lulu ambaye kwa zaidi ya miezi saba yupo mahabusu katika gereza la Segerea anakabiliwa na kesi ya mauaji dhidi ya marehemu Steven Kanumba.

Akiongea na Clouds FM leo katika mahakama kuu ya Tanzania ambapo kesi hiyo inasikilizwa, Dr Cheni ambaye yupo karibu na familia ya Lulu katika kipindi chote cha kesi hiyo amesema masharti yote ya dhamana hiyo yanatekelezeka.

“Kwa mfano kama hiyo wamesema kwamba kuna dhamana ya milioni 20 na mtu mwingine milioni 20 mimi ninaweza nikajitoa katika mmoja wapo katika upande huo,” alisema Cheni.

“Masharti mengine sidhani kama ni magumu kwasababu kila kitu kiko okay sidhani kama kitashindikana sasa hatujajua msajili atakapopata anatoa leo ama atamtoa lini sababu na yeye lazima apate muda wa kupitia yawezekana ana mafaili mengi juu ya meza.”

Cheni amesema masharti hayo yaliyowekwa wanaweza kuyatimiza leo hii. Masharti mengine ya dhamana hiyo ni pamoja na Lulu kurudisha hati yake ya kusafiria, haruhusiwi kutoka nje ya Dar es Salaam na atatakuwa kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya mwezi.