SAA- TIME
GENERATION FM ONLINE
Monday, October 15, 2012
ZAMBI AWA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MBEYA
WEMA SEPETU NA AUNT EZEKIEL WAOMBA RADHI KWA PICHA ZAO MBAYA ZA FIESTA
Waigizaji wa filamu nchini Wema Sepetu na Aunt Ezekiel
wamewaomba radhi watanzania kwa picha zao mbaya walizopigwa kwenye show za
Fiesta.
Wasanii hao wamezungumza na waandishi wa habari kwenye
ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuomba radhi kwa
kupigwa picha hizo za nusu utupu walizopigwa kwenye show hizo.
Wakiongena waandishi wa habari Aunty Ezekiel amesema ameumizwa
na kitendo hicho kwakuwa wao kama wanawake
katika jamii, wana wazazi, ndugu jamaa, marafiki pamoja na mashabiki wao
wanaowapenda na kuwaheshimu.
Hivi karibu Aunty Ezekiel alijitetea na kunukuliwa kwenye
chanzo kimoja akisema, “Ni kweli nilikuwa ninacheza katika Jukwaa (Stage) na
nilikuwa nimekunywa, lakini sikuwa nimedhamiria kukaa uchi bali ni mbinu za
wapiga picha ambao walitumia njia ya kuamua kunidhalilisha kwa kunipiga picha
wakiwa chini ya Jukwaa (Stage) ili wapate kuuza magazeti yao ,
hata ukiangalia picha zenyewe zimepigwa kiujanja sana .”
Waigizaji hao waliongozana na katibu Mkuu wa shirikisho la
filamu Tanzania ,
TAFF, Wilson Makubi.
STAMINA KUJA NA ALBAM YENYE NYIMBO 20
Amesema nyimbo nyingi katika albam hiyo zitakuwa na ujumbe
wa kijamii yaani conscious zaidi.
Aliongeza kuwa pamoja na kuwepo kwa nyimbo zake zilizotoka
kama Kabwela, Alisema na Najuta Kubalehe, katika albam hiyo kuna wimbo
aliomshirikisha Fid Q ambaye anamchukulia kama
baba yake kisanaa katika wimbo uitwao Like Father Like Son.
Fid pia atalipia gharama zote za kufanyika kwa video mpya ya
Stamina ambayo hakutaja ni ya wimbo gani.
TANZANIA NAYO YAJIPANGA KUZIZIMA SIMU BANDIA
Taarifa hiyo imetolewa na kaimu meneja mawasiliano wa
mamlaka ya mawasiliano (TCRA) Semu Mwakyanjala ambaye amesema mamlaka hiyo
itaanza kwa kutoa elimu kwa umma kuhusiana na umuhimu wa kununua simu halali.
Ameliambia gazeti la Daily News Jumapili kuwa hatua hiyo
itachukuliwa na nchi zote wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki zikiwemo Rwanda , Uganda
na Burundi .
Kuna taarifa kuwa makampuni mengi ya simu nchini Tanzania
yameupokea mpango huo kwa shingo upande kwa hofu kuwa yatapoteza wateja wengi.
Kwa upande wa tume ya mawasiliano ya Uganda (UCC) hatua hiyo
ya kuzima simu bandia itafanyika mwishoni mwa mwezi November.
Subscribe to:
Posts (Atom)