Wednesday, October 31, 2012

Lord Eyez apelekwa mahakamani lakini ashindwa kupandishwa kizimbani

Rapper wa kundi la Weusi Lord Eyez leo asubuhi alifikishwa mahakamani katika mahakama ya wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaa akitokea mahabusu katika kituo cha polisi cha Oysterbay na kushindwa kupanda kizimbani baada ya hati ya mashtaka kutokidhi mahitaji ya kisheria.

Lord Eyez alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa tatu asubuhi katika defender, chini ya ulinzi mkali wa polisi na kupelekwa moja kwa moja mahabusu akifichwa asionekane hadharani kwa waandishi wa habari ambao walijazana kwa wingi katika eneo la mahakama hiyo.

Aidha, shauku ya watu wote waliokuwepo mahala hapo ilipotea pale walipopata taarifa kwamba msanii huyo hatapandishwa mahakamani kwa kuwa hati yake ya mashataka ilikuwa na makosa tofauti na anayotuhumiwa nayo, hivyo kuhitajika kufanyiwa marekebisho kabla ya kupelekwa kwa mwanasheria mkuu na kurudishwa mahakamani kwa ajili ya kupangiwa siku ya msanii huyo kufikishwa mahakamani tena.

Kutokana na ulinzi mkali, ilikuwa ngumu kupata picha zake.

H.Baba: Diamond katuma watu waibe flash yenye wimbo alioiba idea yangu


Scandal inayohusiana na wimbo mpya wa Diamond ‘Nataka Kulewa’ imeendelea kuchukua sura mpya baada ya H.Baba leo kuiambia Bongo5 kuwa Diamond Platnumz ameanza kutuma watu wake ili waiibe flash yenye wimbo wake (H baba) ili kusiwepo ushahidi.

“Ninayo kwenye flash lakini siwezi kuiacha sehemu yoyote sababu ameshatengeneza mpaka watu waibe hii flash, yaani sasa ni michongo tu ya ajabu ajabu inaendelea sasa hivi,” amesema.

‘Kwasababu kule studio yaani verse zote zimefutika lakini mimi nilikuwa nayo kwenye flash yaani ile demo nilichukua kwaajili ya kusikiliza nyumbani, studio verse zote zimepotea, huwezi amini.”

Amesema hana lengo la kuuachia wimbo huo lakini atatoa kipande kifupi ili watu wasikie kile anachokisema.

Msanii huyo anasema Diamond alimkuta kwenye studio ya G Records wakifanya wimbo wenye jina hilo (Nataka Kulewa) ambapo Q-Chief aliimba chorus na Diamond kuusifia sana.

Mzungu Kichaa kuendesha semina ya siku mbili kwa wasanii wachanga jijini Nairobi


Mwanamuziki raia wa Denmark mwenye makazi yake nchini Tanzania, Espen Sørensen aka Mzungu Kichaa leo anatarajia kuanza semina ya siku mbili kwa wasanii wachanga jijini Nairobi Kenya.

Semina hiyo itafanyika katika ofisi za Sarakasi Trust.

“The workshop will be steps to success through management, marketing and identity,” yamesema maelezo yake.

Pia Mzungu Kichaa atafanya concert ya bure katika bweni la Sarakasi Ijumaa hii.