Ronan Patrick John Keating alias Ronan Keating
Ronan Keating akiwa na mpenzi wake mpya.
Ronan Patrick John Keating alias Ronan Keating mwanamuziki
maarufu toka Ireland na pia mtunzi wa nyimbo ambaye ameshatamba na single zake
kama “This I Promise You” na “When You Say Nothing” kwa sasa ameanza kupata
furaha ya mapenzi baada ya kupata mpenzi mpya.
Mpenzi wake mpya huyo anajulikana kama Storm Uechtritz,
Keating na Storm walianza mahusiano mara baada ya kutengana na mpenzi wake wa
awali.
Ronan Keating ambaye alishawahi kuwa mmoja wa wanamuziki wa
kundi la Boyzone amepata mpenzi mwingine
wakati akiwa katika X-Factor huko Australia ambako alikuwa ni muandaaji. Ronan
mwenye miaka 35 sasa ndoa yake ya miaka 14 na Yvonne iliisha rasmi Aprili mwaka
huu kutokana na kashfa iliyomkuta kwa kufanya mapenzi na dansa wake.
No comments:
Post a Comment