Wednesday, January 30, 2013

Maoni: TID na Wema Sepetu wapendekezwa zaidi kuiwakilisha TZ kwenye BBA 2013, mnyama asema atachukua fomu



Tarehe 26 tuliandika habari kuhusu Mastaa 10 wanaoweza kuwa wawakilishi wazuri wa Tanzania katika shindano la Big Brother Africa 2013. Katika majina hayo 10, Wema Sepetu, TID, Lisa Jensen na Fezza Kessy ndio walionekana kuwavutia wengi.

Leo kupitia ukurasa wetu wa Facebook tumeendesha kura ya maoni ambapo tumewataka watu wawataje mastaa kati ya hao wanne wanaoweza kuwa wawakilishi wazuri wa Tanzania. Katika kura hizo zaidi ya 800 TID na Wema ndio walioongoza kwa kutajwa zaidi.

Baada ya matokeo hayo tumempigia simu TID kumpa taarifa hiyo aliyoipokea kwa furaha kubwa na kudai kuwa hiyo ni ishara ya jinsi anavyokubalika kwa mashabiki.Tulipomuuliza kama atafikiria kuchukua fomu kwaajili ya kujaribu bahati yake, Top in Dar amesema kwakuwa watanzania wamemtaka afanye hivyo basi ataenda kuchukua.

Tunafanya jitihada kupata msimamo wa Wema pia.Tazama maoni hayo hapa:

http://www.facebook.com/photo.php?fbid=529169297116509&set=a.296410577059050.80456.107179369315506&type=1&theater

Lulu aziteka ‘frontpage’ za magazeti ya leo (Jan 30)


Picha za msanii wa filamu Elizabeth Michael maarufu Lulu ambaye jana alitoka nje kwa dhamana, zimeyateka karibu magazeti yote ya Tanzania ya leo.

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemwachia kwa dhamana Lulu aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kumuua msanii mwenzake wa filamu Steven Kanumba Aprili 7, 2012 bila kukusudia baada ya kukamilisha taratibu zote za dhamana.

Masharti ya dhamana hiyo ni kutakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao ni wafanyakazi wa serikali waliotakiwa kutoa shilingi milioni 20 kila mmoja. Mengine pamoja na Lulu kurudisha hati yake ya kusafiria, haruhusiwi kutoka nje ya Dar es Salaam na atatakuwa kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya mwezi.

Magazeti yote ya Kiswahili na Kiingereza a Tanzania yameandika habari hiyo ama kuweka picha za Lulu baada ya dhamana yake kukamilika jana.Picha nyingi zinamuonesha Lulu akilia kwa furaha huku akiwa bega kwa bega na mama yake mzazi.