Leo hii rapper kutoka Mbeya Emmanuel Simwinga aka Izzo B, ameachia ngoma mpya iitwayo Ball Player akiwa na Quick Rocka na Ngwair.
Beat ya ngoma hii imetengenezwa na Nahreel na nirahisi kusikia touch za kipekee za beatmaker huyo hasa zile brass zinasosikika vizuri kwenye chorus iliyoimbwa na Quick Rocka pamoja na zile drums zinazosikika kama zimepigwa live, design kama beat za Just Blaze. Lamar ndiye aliyemalizia vocals na mixing.
Katika verse ya kwanza ya Ball Player, Izzo B anazungumza jinsi alivyotoka mbali kwa kuja Dar kuifuata ndoto yake ya muziki na kufikia kwa washkaji. “Nimekuja Dar sina ghetto ila now naishi kwangu,” anasema na kuzungumzia jinsi mambo yalivyo safi sasa hivi.
Verse ya pili anaingia Ngwair na kama kawaida yake swagga zinakuwa on. “Mi nahustle hard ndio swagga zangu everyday, Big Beats zinahit kwa streets bila Dre”.Anazungumzia jinsi ambavyo muziki anaudai na wala hashtushwi na watu wanavyomponda.“Usiongeongee hizi dis.com nilishazizoea, unaweza kupaka unavyotaka mimi sijali ukininyea”
Verse ya pili Izzo anarejea na anaendelea na tambo na kisha kuwachana wasanii wakongwe. “Salute kwa kaka zetu japo wachache wenye love, Hawatupendi sisi wa sasa kumbe kisa cha kipumbavu.