Saturday, November 24, 2012

Chezea Tuzo; AY Ampiku Diamond Kufanya Kolabo Na J Martins



Kwa wale ambao walikuwa wakifuatilia kwa karibu, habari za msanii Diamond kwa kipindi kirefu cha mwaka huu watapata kushangaa nini kimetokea kwa kolabo yake na msanii J Martins ambayo amekuwa akiitangaza mara kwa mara huko nyuma.


Well kwa sasa inaonekana msanii huyo kutoka Nigeria atafanya kazi na msanii aliyepata tuzo ya video bora Afrika Mashariki kupitia Kolabo na wasanii wa Kenya Sauti Sol, Ay na swahiba wake wa karibu Mwana FA.
Kwa mujibu wa tetesi za chinichini, mipango yote ya kolabo hiyo imeshaiva na pengine kazi hiyo ikakamilika siku si nyingi.
Well tusubiri na tuone yatakayojiri.

Sajuki Kuwashukuru Watanzania Live Kwa Mara ya Kwanza Iringa


KATIKA kutoa shukrani kwa Watanzania wote waliowajibika katika kuhakikisha wanamsaidia mwigizaji na mtayarishaji mahiri wa filamu kutoka Swahiliwood Juma Kilowoko ‘Sajuki’ kupatiwa matibabu kutokana na maradhi ya tumbo na kwenda kutibiwa Nchini India na kupona, kampuni ya Wajey Film Company imeandaa tamasha kubwa la shukrani.
Ni tamasha la aina yake kutokana wa wadau wafilamu na Watanzania kwa ujumla kufurahia kurudi kwa sajuki katika hali yake ya mwanzo, Stara alisema onyesho hilo litafanyika kwa ajili ya kukusanya fedha zitakazopelekwa kwa wasanii wanaosumbuliwa na maradhi na kukosa matibabu alisisitiza mratibu huyo.
Bongo5 iliongea na mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo mahiri katika utengenezaji wa filamu, Wastara Juma ‘Stara’ amesema kuwa baada ya mumewe Sajuki kupata matibabu anatumia fursa hiyo katika kuwashukru watanzania waliojitoa kwa hali na mali katika kufanikisha matibabu hayo.
kama familia hatuna cha kuwalipa watanzania kwa moyo wao wa upendo walioonyesha kwetu, katika kipindi kigumu na majaribu wakati Sajuki akiwa anaugua, si rahisi kumfikia kila mtu kwa wakati mmoja lakini kwa njia ya tamasha hilo tutawafikia, tunawapenda watanzania mungu awabariki sana,”anasema Wastara.
Tamasha hilo linatarajia kufanyika siku ya jumapili Tarehe 25/11/2012 katika uwanja wa Samora huku wasanii wa muziki wakitumbuiza kwa nguvu Mzee Yusuf, Linah, H. Baba na mchekeshaji Kitale ataimba burudani kubwa ni pale mechi kali itakapopigwa kati ya wasanii nyota wa filamu kutoka Bongo movie na timu kali ya watangazaji wa redio zote mkoani Iringa.

Ni kweli Keri Hilson aliidiss Afrika kwa kutuita starving Africans?

Huenda Keri Hilson akaja Tanzania na Kenya katikati ya mwezi ujao (December) akiwa tayari amewakera waafrika kwa tweet yake ambayo yeye anasema hakuiandika. Tweet hiyo inayotuponda waafrika kuwa tunakufa na njaa.

Katika tweet hiyo Keri aliandika, “IT’S THANKSGIVING ! Just did that 19 hour flight back from Ghana and most definitely am going to eat like a pig for the starving Africans.”

Tweet hiyo iliamsha hasira kubwa wa waafrika waliochukizwa na kitendo cha msanii huyo kulidharau bara la Afrika kiasi hicho.

Jana imemlazimu msanii huyo kukanusha kuandika tweet hiyo kwa madai kuwa kuna mtu aliitengeneza kwa kutumia program ya photoshop ili kumkosanisha na waafrika.

“Wow. People actually believe I’d say that? I woke up & saw a fake photoshopped tweet abt me dissing Africa?! C’mon man. Really? Disgusting.

“REALLY didn’t wanna spend any part of my day combating foolishness But I simply cannot hv u doubting my sincerity abt my love for Africa!”

“And for those still skeptical, I wasn’t even in Ghana this trip. They didn’t even have the facts right to make it believable.”

Tumwamini nani?

Avril wa Kenya kuja na ear/headphones zake



Msanii wa kike wa nchini Kenya, Avril ameamua kuonesha kuwa biashara ya headphones inaweza kufanywa na msichana pia kwa kuanzisha aina ya ear/headphones zake ambazo kama zikiwa na ubora mzuri huenda kwenye soko la Afrika Mashariki zikatoa upinzani kwa zile za Dr Dre Beats By Dre.

Hata hivyo mradi wake huo utapewa shavu na wizara ya elimu ya juu, sayansi na teknolojia ya nchini Kenya.

Ear phones hizo zitajulikana kama Gs N Fs na zitakuwa sehemu ya mradi wa kuwainua vijana wenye vipaji na mawazo kuhusiana na teknolojia ambao hawana rasilimali za kuendeleza vipaji vyao.

Picture of the day: AY akipokelewa airport kama kiongozi wa nchi




Kwa kazi aliyoifanya kwenye CHOMVA 2012, AY anastahili mapokezi kama haya. Welcome back home boy.