Unakumbuka tuliwahi kuandika kuwa baada ya Rick Ross kupiga show kwenye Fiesta mwaka huu kuna msanii mwingine mkubwa anaweza kuja Tanzania hivi karibuni? Well, msanii huyo anaweza kuwa ni Chris Brown…. Yesss Breezy huyu huyu ex wa mtoto Rihanna.
Issue ni kwamba mwezi December mwaka huu kampuni maarufu ya uaandaji wa show nchini Afrika Kusini pamoja na Channel O watamdondosha Chris kwenye ‘Carpe Diem Tour’ ambapo kampuni kubwa ya Tanzania inadaiwa kuweza kutumia nafasi hiyo pia kumdondosha Breezy ndani ya Dar es Salaam.
Chris atakuwa na show Johannesburg, December, 15, Durban December, 17 na Cape Town December 19 na December 20.