Jamie Foxx.
Sababu pekee inayofanya Jamie asitake kuonana wala kumsamehe baba yake ambae ana umri wa miaka 74 ni kutokana na mzazi huyo kumtelekeza akiwa mdogo.
Jamie alilelewa na bibi yake ambae alifariki mwaka 2004, toka mwaka huo Jamie hajawahi kuongea na baba yake mzazi.
Kwa sasa baba yake mzazi ni mgonjwa sana na amekua akihitaji kuonana na Jamie ili wayamaliza lakini staa huyu amekataa.
Mke wa sasa wa baba yake Jamie amekaririwa akisema “tumekua tukimpigia simu Jamie kwa miaka sasa lakini hapokei na wala hajawahi kujibu mamia ya msg tulizomuandikia, na sasa baba yake ni mgonjwa na anapumulia mashine… natamani Jamie apige simu”
Ni mastaa wengi wa dunia mpaka sasa ambao wamekua kwenye uhusiano mbaya na baba zao akiwemo Beyonce, Kelly Rowland nae alikua haongei na baba yake, movie star Angelina Jolie mpaka sasa bado hayuko kwenye uhusiano mzuri na baba mzazi.