Sunday, December 2, 2012

Video: Jua walichoongea Dude na Sharomilionea kabla ya kupoteza maisha



Mwigizaji Dude amefunguka kuhusu maongezi yake na marehemu Sharo Milionea kabla ya ajali kutokea, msikilize hapa.

wimbo wa all stars kama kumbukumbu ya SHARO MILLIONEA

Fid Q amtambulisha dogo aliyemfunda kwa miezi 9

Fid Q


Mwanamuziki mkongwe wa Hip hop Fid Q , almaarufu kama Ngosha the Don, amesema ameamua kumchukua mwanafunzi mmoja na kumfundisha Muziki ili mwanafunzi huyo aweze kupambana na ushindani mkubwa uliopo kutoka kwa wasanii mbali mbali kwenye Muziki.

Akiongea kupitia kituo kimoja cha Radio leo jijini Dar-Es-Salaam, Fid Q alisema anaona fahari kuwa msanii anayetoa fursa kwa vijana badala ya wao (vijana) kumtegemea kwa kolabo ama pesa lakini kwa kuwafunda yeye mwenyewe wataweza kujihudumia wenyewe katika siku za baadae.

Fid Q amekuwa mfano mzuri sana wa kuigwa katika ubunifu na moyo wa kujitolea, na katika siku za hivi karibuni kupitia mahojiano tuliyoyafanya naye msanii Stamina, alionyesha kumkubali sana Fid Q, na kusema ni mtu anayemtegemgea kwenye Muziki wa Hip Hop kwa sababu anamuona kama ni nguzo na msingi wa Hip Hop hapa bongo.

Stamina alisema “kama kuna msanii ambaye ninamkubali sana, basi ni Fid Q , kwani ni msanii pekee aliyesoma vitabu vingi sana ndiyo maana haishiwi mashairi, pamoja na uwezo wake wa kuchana.
Aidha Fid Q alisema mwanzoni aliwawachukua vijana 6 ambao bado walikuwa hawajakomaa, kwa hiyo akawafanya kama wanafunzi na kuwafundisha muziki, na hatimae sasa mmoja wao amemaliza masomo na na kuwa msanii ambaye aliyeiva kimuziki.

Fid Q alisema “nimeamua kuwafundisha vijana muziki ili wawe na uwezo kama wangu na kuwapa fursa katika maisha yao kwa sababu ni vigumu sana mtu kumpa kazi ambayo itamsaidia kimaisha ila ukimpa fursa utamsaidia sana kuliko kumpa pesa. Alimalizia.