Jana wapenzi waliorudiana rasmi, Chris Brown na Rihanna walionekana wakitoka pamoja nyumbani kuelekea mahakamani jijini Los Angeles.Rihanna alikuwa amevaa sunglasses na mara nyingi alikuwa ameinama chini kuziba uso wake.
Wapenzi hao walisindikizwa na mama yake Chris Joyce Hawkins wakati huu ambao Brown anadaiwa kudanganya masaa ya kazi alizozifanya kwenye jamii kama sehemu ya probation yake kufuatia kesi ya kumpiga Rihanna mwaka 2009.
Wakili wa Brown Mark Geragos na polisi wa Richmond Virginia wamekanusha madai hayo. Akiongea na waandishi wa habari jana Geragos alisema: Sijawahi kuwa na mteja aliyeteswa kama Chris Brown.
Wakili wa Brown Mark Geragos na polisi wa Richmond Virginia wamekanusha madai hayo. Akiongea na waandishi wa habari jana Geragos alisema: Sijawahi kuwa na mteja aliyeteswa kama Chris Brown.
Chris akiwa mahakamani
Aliongeza kuwa Rihanna alimsindikiza Brown mahakamani na hajafurahishwa na madai hayo mapya.