Wednesday, November 14, 2012

Mamia wamuaga marehemu Mariam Khamis




Mamia ya watu leo wamejitokeza katika mazishi ya muimbaji mahiri wa Taarab nchini Mariam Khamis maarufu kama Paka Mapepe aliyefariki juzi wakati akijifungua. Mariam alifariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo mtoto wake alisalimika.
Marehemu Mariam Khamis

Mazishi hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu wa aina mbalimbali wakiwemo wasanii wengine wa muziki wa Taarab.

Miongoni mwa wasanii waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Khadija Kopa, Isha Mashauzi, Mzee Yusuph na mke wake Bi Leila,Nyota Waziri, Bi Hindu na wasanii wenzake wa kundi la TOT.
  

Mariam alikuwa muimbaji wa kundi la taarab la TOT na enzi za uhai wake aliwahi kuimbia katika makundi mbalimbali ya taarab ambayo ni pamoja na East Africa Melody, Zanzibar Stars na 5 Stars.

Marehemu Mariam Khamis ameimba nyimbo nyingi zinazofanya vizuri katika muziki wa Taarab zikiwemo ‘Huliwezi bifu’, ‘Raha ya Mapenzi’ na ‘Ndo basi tena’.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pepa peponi.



Nauli ya ndege kama ya basi!! FastJet kuanza safari zake kwa kishindo


Kampuni ya ndege ya FastJet imeanza rasmi kuuza tiketi za ndege kwa safari za ndani ya nchi ambapo safari zitaanza November, 29.Kilimanjaro na Mwanza ni mikoa ya

Bhoke (BBA) ateuliwa kuwa balozi wa taasisi inayopambana na funza wa miguu (jiggers)


Aliyewahi kuwa mwakilishi wa Tanzania katika shindano la Big Brother Africa, 2011, Bhoke Egina ameteuliwa kuwa balozi mpya wa Tanzania wa taasisi ya Ahadi Trust Tanzania.

Jordin Sparks azindua perfume yake ya pili kwa picha za nguvu


Mrembo na mwanamuziki wa R&B wa nchini Marekani, Jordin Sparks anazindua perfume yake ya pili. Katika kuitaganza perfume hiyo iitwayo Ambition mrembo huyo ameambatanisha na picha za kuvutia zinazodhihirisha jinsi alivyo mrembo.

Song : Ali Kiba – My Everything



My Everything – Alikiba (Lyrics)
Verse 1