Friday, November 2, 2012

ALICHO SEMA PASHA KUHUSU DIAMONDI HIKI HAPA

Kutokana na skendo iliyo hit sasa hivi Bongo kutokana na msanii alieonekana kughara ghafra katika game ya muziki wa bongo flava na kutazamwa kwa macho mengi zaidi na utofauti wake, moja kati ya wasanii wakongwe katika Game na  ambae amekumbwa na mkasa huu kwa kuibiwa Beat yake pamoja na melod ya Corus yule hit maker wa NISOO (PASHA) ameweka picha hii katika ukurasa wake wa Facebook na kuandika maneno haya.....

(Mdogo wangu Diamond umekwama wapi kakazako tukusaidie@wakongwe katika game,,,,,!!!!???? 

Kazi kwako Diamond Plutnumz Baibeeeeeeee..........


Exclusive: Barnaba azungumzia sababu za kushindwa kuhudhuria show ya Africa Unplugged

Mwishoni mwa mwezi August mwaka huu Barnaba alikuwa msanii pekee wa Tanzania aliyechaguliwa kwenda kuperform kwenye show kubwa iliyopewa jina la Africa Unplugged jijini London Uingereza.

Barnaba ameiambia Bongo5 kuwa sababu za kushindwa kuhudhuria show hiyo ni kukosa visa ya kwenda nchini Uingereza.

“Sikwenda kwasababu passport yangu ilicheleweshwa kutokana na ubalozi wa UK ambao uko Tanzania makao makuu yake ni Nairobi kitu ambacho mimi kama mtanzania sikukipenda pia why ubalozi wetu wa UK uwekwe Nairobi? Kwanini wa Nairobi usibaki Nairobi wa Tanzania usibaki Tanzania? Hicho ni kitu ambacho kimenidisappoint pia. Kusubiri visa yangu ambayo nilitakiwa nisubiri ilibidi nisubiri siku 14 na siku za safari zilibaki saba kwahiyo nilichelewa siku saba mbele yake, ilibidi niikose show. Iliniathiri sababu ilikuwa bonge la opportunity inawezekana ningepata mlango mwingine na kunifanya kuwa mkubwa. Nilitegemea kulipwa lakini hata kama nisingelipwa, malipo yangu ya kupata nafasi kubwa zaidi ya kazi nyingine nafikiri ilikuwa kubwa kuzidi hata ile percent ambayo ningepata.

Kuhusu kuchelewa kufanyika kwa collabo yake na Fally Ipupa

Collabo ya mimi na Fally Ipupa ipo lakini nafikiri connection kidogo imekuwa ngumu kutokana na mtu mwenyewe ni mkubwa amekuwa na mambo mengi ana tour nyingi na mihangaiko inayonitinga hapa Tanzania ni mingi kwahiyo sina cha kusema sana kwa sasa mpaka nitakapoifuatilia tena hii issue lakini mawasiliano yapo na connection kubwa ipo.

Wakati huo huo Jumanne ijayo Barnaba ataachia wimbo mpya alioupa jina la Sorry ambapo amesema: “Ni nyimbo yangu mpya kabisa ambayo naamini inaweza kubadilisha soko la muziki wa kitanzania. Nyimbo imetengenezwa na watu wengi producer ni Imma the Boy imetengenezwa pale THT , mwandishi ni mimi mwenyewe Barnaba lakini watu wengi wameshiriki.”

Amewataja wengine walioshiriki kuwa ni pamoja na Ditto, Mwasiti, Waziri Njenje, Kardinal Gentle.

Aslay: Nimezifahamu tuzo za Kora jana

Msanii wa hit ya Nakusemea, Aslay ambaye ametajwa kuwania katika tuzo zenye thamani kubwa barani Afrika za Kora, Aslay, amesema alikuwa hazifahamu tuzo hizo hadi jana.

Akiongea kwa simu na Bongo5 Aslay amesema alipoambiwa kwa mara ya kwanza hakuamini na baada ya kuambiwa ukubwa wa tuzo hizo alikuwa na furaha isiyoelezeka.

“Mara ya kwanza ile nilikuwa sifahamu, nimezifahamu jana hiyo hiyo watu ndio wananiambia bwana tuzo kubwa sana hizo,” amesema.

“Najisikia vizuri kwasababu namshukuru mwenyezi Mungu kwanza kwa nilikotoka mpaka hapa nilipofika kwahiyo nina furaha tu.”

Aslay ametajwa kuwania kipengele cha msanii anayechupikia barani Afrika.

Exclusive: Sikiliza ‘Nataka Kulewa’ ya H.Baba anayodai Diamond ameiba idea


H.baba ametuletea exclusively kipande cha wimbo wake uitwao ‘Nataka Kulewa’ ambao amemshirikisha Q-Chief. Msanii huyo anamshutumu Diamond kuiba wazo na jina la wimbo wake huo katika wimbo wake mpya wenye jina kama hilo.

Tumefanya naye mahojiano ambayo utayaangalia muda mfupi ujao kupitia hapa hapa lakini kwa sasa usikilize wimbo huo hapa ambao bado ni demo.

Jackline Wolper ‘alia’ na wabaya wake baada ya gari lake kuchomwa moto

 Usiku wa kuamkia tarehe 23 mwezi uliopita watu wasiojulikana walilichoma kwa moto gari la Jackline Wolper lililokuwa limepakiwa nyumbani kwake. Hata hivyo gari hili halikuungua lote.
 Gari la Jackline baada ya kuchomwa

Kupitia blog yake, Jack ameandika:

Kiukweli mimi kama Jacquline Wolper sina ubaya na mtu yeyote, ila nmeshangaa kuona watu nisiyo wajua kuja usiku wa manane na kunichomea gari yangu. Kiukweli siwezi kumuhisi mtu ila najua ni lazima atakua mtu asiependa maendeleo yangu ni ni mtu mbaya sana kwangu. Na inawezekana kabisa alipanga kunia lakni kwa bahati nzuri siku hiyo sikua nyumbani nilikua nimesafiri. Tukio lilitokea usiku wa tarehe 23/10/2012 ambapo mtu alitumia matambara yaliyo na mafuta ya taa au Petrol akiwa kwa nje ya ukuta wa nyumba yangu akiwa anarusha kwa ndani. Nimepeleka taarifa kituo cha Polisi kawe kwa kutaka msaada wa kiupelezi na nitakua nawapa taarifa za kila kinachoendelea. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwani niko salama.

Pole Jackline.

Wamarekani wachukizwa na kitendo cha Chris Brown kuvaa kama Taliban kwenye Halloween party ya Rihanna

Kwa mara nyingine tena leo kumeshuhudiwa machafuko mengine katika mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam baada ya polisi wa FFU kutumia mabomu ya machozi kulitawanyisha kundi kubwa la waumini wa dini ya kiislam waliokuwa wanaokena kutaka kuandamana.

Juzi Rihanna aliandaa party ya Halloween huko West Hollywood na kukaribisha mastaa kibao akiwemo swahiba wake Chris Brown.

Chris ndiye aliyezua mjadala kutokana na kuvaa kama wanamgambo wa Taliban. Akiwa amevaa nguo hizo Chris alivaa pia mkanda wa risasi kifuani mwake pamoja na kushikilia machine gun huku akipewa kampani na washkaji zake waliokuwa wamevaa kama yeye.
Chris Brown (katikati) akiwa na washkaji zake

Aliweka picha hiyo kwenye mtandao wa Instagram na kuandika “Ain’t nobody F**king wit my clique!!!!”

Mastaa wengine waliohudhuria party hiyo ni pamoja na Flo Rida, Paris Hilton, na staa wa Olympic Lindsay Vonn.

Baada ya watu kumshambulia Chris kwa kitendo hicho cha kuwaunga mkono magaidi mama yake Joyce Hawkins alimtetea mwanae kwa kuandika, “HALLOWEEN IS FOR FUN NOTHING MORE THAN JUST FUN. GET A LIFE PLEASE.”