Tuesday, September 11, 2012

Usafiri wa treni Dar waanza kwa majaribio jana



TATIZO la kugombania daladala katika baadhi ya maeneo jijini Dar es salaam litapungua hivi karibuni baada ya majaribio ya usafiri wa treni kuanza
Jana majaribio ya usafiri huo yalianza na wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuonekana kuufurahia usafiri huo mabao unaonekana utakuwa mkombozi wa msongamano wa magari.

Majaribio hayo yaliongozwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi Bw. Charles Tizeba, ambapo treni hiyo ilitoka Posta hadi Ubungo

Naibu Waziri huyo alisema, usafiri huo unatarajiwa kuanza rasmi Oktoba mwaka huu baada ya kutathmini bajeti nzima ya uendeshwaji na kujua bei ya nauli kwa wateja ambao watatumia usafiri huo.

Alisema wakazi wasiwe na wasiwasi usafiri huo upo na sasa kuna marekebisho madogo katika reli hiyo ambapo usafiri huo

Alisema kila behewa litakuwa na uwezo wa kuchukua abiria 900 na treni hiyo itafanya safari zake mara tatu kwa siku