Thursday, November 22, 2012

Said Salim Bakhresa akamata nafasi ya 30 katika orodha ya watu matajiri 40 barani Afrika – Forbes


Bakhresa (kulia) alipokuwa akisalimiana na rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein

Orodha ya jarida la Forbes la watu 40 matajiri zaidi barani Afrika imetupa jibu la ‘uhakika’ nani ni mtu tajiri zaidi kuliko wote nchini Tanzania. Si mwingine zaidi ya Said Salim Bakhresa ambaye amekamata nafasi ya 30 kati ya matajiri 40 wa barani Afrika kwa kuwa na utajiri unaofikia dola milioni 520 hadi kufikia November, 2012.

Bakhresa ana historia ya pekee kwa kuacha shule akiwa na miaka 14 na kujiingiza kwenye biashara ndogo ndogo ikiwa pamoja na mgahawa na biashara ya unga wa kusaga.

Leo hii Bakhresa Group imeajiri zaidi ya watu 2,000 na ni kampuni kubwa zaidi Tanzania. Bidhaa zake zina umaarufu mno nchini na nje ya nchi ambazo ni pamoja na unga, vinywaji, ice cream, usafiri wa meli na mafuta miongoni mwa nyingine.

Kampuni ya Bakhresa ni wazalishaji wakubwa zaidi wa unga wa ngano Afrika Mashariki na kati ambayo huzalisha kiasi cha 3,200 za tani za metric. Kampuni yake huendeshwa na wanae wa kiume waliogawana vitengo mbalimbali.

Angalia list nzima hapa:

http://www.forbes.com/africa-billionaires/list/

Song : Amazon – Mamito





Ni Mikosi Mfululizo Kwa Msanii Barnaba



Msanii Barnaba Elias ambaye anajulikana kwa sasa kama Baba Steve amekumbwa na maswahibu mfululizo ambayo itambidi kuwa makini la sivyo na yeye ataingia kwenye vitabu vya wasanii ambao wanakumbwa na mikasa inayoweza kumpelekea kukosa mwelekeo wa kimuziki.

Kwa mujibu wa habari ambazo zipo kitaani msanii huyo alikumbwa na mkasa wa kwanza siku ya Jumapili iliyopita katika klabu ya usiku ya Club Billicanas ambapo wakati anatumbuiza kukatokea tukio la kusikitisha lililopelekea mpenzi wake, ambaye anajulikana kama Mama Steve kuswekwa lupango kwa kumpiga chupa msichana ambaye inasemekana alikuwa mpenzi wa zamani wa Barnaba aliyekuwa akionyesha ishara za wazi wazi za kimapenzi.

Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari vilivyokuwepo katika Club hiyo ya usiku, baada ya kuona hivyo, Mama Steve alichukua chupa na kumpiga nayo msichana huyo ambaye alipasuka vibaya usoni na kuwahishwa polisi na kisha hospitali ili kupata matibabu, na kisha Mama steve ambaye ndiye mpenzi wa Barnaba kupelekwa katika kituo cha polisi Oysterbay ambapo inasemekana kuna maridhiano kati ya pande zote tatu na kila kitu kinakwenda sawa.

Baada ya tukio hilo, inadaiwa kuwa kuna msichana mwingine anayeishi maeneo ya Mwananyamala wilaya ya Kinondoni ambaye anamtafuta Barnaba ili ambwagie mtoto kwakuwa anadai amekuwa hampi sapoti yoyote katika matunzo.

Binti huyo, inavyosemekana anatafuta nafasi ambapo msanii huyo atakuwa na shoo na yeye atatafuta upenyo wa kwenda kumbwagia mtoto huyo!!

Tunachojaribu kujiuliza hatujui ni mdudu gani aliyeingia katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya husasan Bongo Flava kwakuwa ‘trends’ za sasa zinaonyesha matukio yasiyo ya kawaida kwa wasanii wetu yameendelea kushika kasi na hili la Barnaba ni moja ya vitu vinavyotufanya tujiulize, je! kama itatokea hivyo mambo hayo hayawezi kupoteza focus ya msanii? Au wasanii wanaoonekana kukomaa na hivyo kuzima nyota zao za kisanii wakiwa bado hawajadumu vya kutosha?

Breaking News: Muigizaji Mlopelo Asemekana Kufariki Dunia



Muigizaji mahiri ambaye alikuwa anatamba katika kundi la Kaole Sanaa Group Mlopelo anasemekana amefariki dunia siku ya leo. Kwa mujibu wa taarifa ambazo pia bongo5 inajaribu kuzithibitisha kutoka kwa mmoja wa wana tasnia ya filamu Pastor Myamba, ambaye naye ametupasha kupata taarifa za kifo chake kupitia ujumbe mfupo wa maneno.
Inasemekana Chanzo cha kifo chake ni maradhi ya muda mrefu.
Mlopelo mara nyingi alikuwa anaigiza kama zezeta la msukule na kujipatia umaarufu mkubwa kutoka kwa wapenzi na tamthilia za kitanzania ambazo mara nyingi zilikuwa zinaonekana kupitia ITV na Channel Ten.
Bongo5 inajaribu kufuatilia habari hii kwa kina zaidi.