Tuesday, February 5, 2013

Zola D kuanzisha kipindi cha TV cha mazoezi!



Hivi karibuni Bongo5 ilichat na rapper na bondia nchini Tanzania, Zola D ambaye alisema ana mpango wa kuanzisha kipindi cha TV.

“Now nina mpango wakuanzisha kipindi cha TV pia na kurusha video zangu za mazoezi kwenye Youtube ili kila mtu alie nyumbani aweze kufanya mazoezi sio mpaka uingie gym, “ alisema Zola.

“Mimi siendi gym kufanya mazoezi nafanya home pia gym naenda kama nina game ya boxing,ili niweze kufundishwa na mwalimu mbinu mbali mbali za mapigano na ushindi.”
Zola akiwa na P-Funk

Akijibu swali la ni vipi ameweza kuujenga mwili wake kiasi hicho, Zola amesema, “Mwili wangu nimeujenga toka miaka mingi sana sasa nina miaka 18 tokea nimeanza kufanya mazoezi ndio maana unaweza kuona mwili wangu umejengeka sana kuliko watu wengine hapa Bongo. Pia mazoezi ninayofanya ni mazoezi ya mapigano na mazoezi ya kujenga nguvu kama push up kukimbia,kuruka kamba,na kufanya swimming sababu napenda sana mazoezi na ndio starehe yangu kubwa,pia nafanya mazoezi kila siku ndio chakula cha maisha yangu,so kila siku nazidi kugain na kuongezeka.”

“Mazoezi yananisaidia sana kwenye afya yangu coz sijaumwa malaria huu ni mwaka wa 4 pia mafua kifua nk,coz ukifanya mazoezi damu inakuwa na nguvu sana,”aliongeza.

Hata hivyo Zola amesema hana pambano lolote hivi karibuni na kuongeza kuwa mchezo wa ndondi kwa Tanzania haulipi.

“Game za Bongo hakuna pesa kabisa ni kuumizana tu promoter wenyewe njaa tu, promoter hana hata baiskeli. Nia yangu ni kupigana ngumi za nje na kuitangaza Tanzania.Nipo tayari kupigana na bondia yoyote mkubwa wa dunia coz najua nina kipaji cha sports pia napenda sana kupigana nikitoka damu ndio naskia raha sana najiona mimi ndio mwanaume.”
Zola na Mad Ice


Kuhusu kuzichapa kiukweli na Mad Ice ambaye pia ni bondia na ameigiza kwenye video yake ya Knock OUT, Zola amesema Ice ni mtoto mdogo.

“Mad ice hawezi kupigana na mimi,pia mimi ni mwalimu wake namfundisha boxing. Nawaomba watanzania wazidi kuniombea dua niweze kutimiza ndoto zangu za kupigana level za kimataifa,muziki wangu level za kimataifa na michezo yangu mingine kama kukimbia mita 100, mita 200,kuruka viunzi,kucheza rugby, kupigana boxing mixed martial arts.”

No comments:

Post a Comment