Monday, November 5, 2012

Obama kutetea kiti chake cha urais kesho?

Wagombea wa urais wa Marekani Barack Obama na Mitt Romney wanaisogelea siku ya uchaguzi huo utakaofanyika kesho kwa kumalizia kampeni zao za mwisho.

Jana Romney alikuwa akizungumza na wapiga kura kwenye jimbo la Pennsylvania ambalo wasaidizi wake wanasisitiza kuwa atalichukua.

Naye Obama alikuwa na mikutano huko New Hampshire na Florida kabla ya jioni kuhutubia kwenye majimbo ya Ohio na Colorado.

Wote Obama na Romney wanakabana koo vilivyo kwa mujibu wa kura za maoni japo kura katika majimbo muhimu zinaonesha Obama kuongoza kidogo.Hata hivyo hakuna kambi iliyo na uhakika wa kushinda hadi sasa.

Prezzo na Goldie wahudhuria engagement party nchini Nigeria

Licha ya hivi karibuni Goldie kukanusha kutokuwa na uhusiano wowote na Prezzo, mastaa hao siku ya November 2 walionekana pamoja kwenye sherehe ya kuvalishana pete ya Olamide na Seun Oyeyip huko jijini Lagos.

Picha hizi zinaamsha tena tetesi kuwa huenda kweli mastaa hawa wakawa na uhusiano tofauti na jinsi wanavyosema wao.

Nuru the Light: Hatutakiwi kunyoosheana vidole bali tumsaidie Ray C

Wakati kila mmoja anayemfamu Ray C anaonekana kusikitishwa na hali aliyonayo sasa kutokana na matumizi ya madawa wa kulevya, msanii wa kike aishiye barani Ulaya, Nuru the Light amesema huu si muda wa kunyoosheana vidole bali kumsaidia tu Ray C arudi kwenye hali yake.

Kupitia blog yaKE Nuru ameandika:

I have worked with people who have been the victims of drugs so I know what she is going through right now. shes not going through it by herself but also the members of her family as well and that is the bad thing about drugs it is the shame that comes with it.

Tanzania as of now hatuna rehab nzuri sidhani ambayo itakayoweza kumsaidia Rehema ila you never know but i do hope with all my body and soul kuwa hatutakiwi kupoint fingers kwa anyone bali tunatakiwa kumsupport na kumsaidia Rehema. In life you don’t know what tomorrow holds but we all hope for the best not only within ourselves but also for our loved ones.

This is a disease na narudia tena huu ni ugonjwa kama vile malaria and needs to be treated ili aweze kuendelea kuishi maisha yake maana sasa hivi issue ni kukomboa maisha yake.

I pray for you Rehema and I love you and this is not going to be easy,this will be one of the hardest things you will go through but i know that you can do it,huwa tunasema Mungu hakupi mzigo usioweza kuubeba na huu ni mtihani ila with God and the love of your mother na wengineo you will get through this!!!

Baada ya Mwanza Mwanza na August 13, Majani na Fid Q waingia jikoni tena

Pamoja na Huyu na Yule iliyofanywa na Master Jay kumtambulisha vema Fid, ni P-Funk Majani ndiye anapewa credits nyingi zaidi za kumweka kwenye chart rapper huyo kutoka Mwanza ambaye jina lake halisi ni Fareed Kubanda. Majani kupitia Bongo Records, ameshafanya hits kadhaa za Fid zikiwemo Mwanza Mwanza, August 13 na Chagua Moja.

Na sasa jamaa hawa wawili wameungana tena ambapo Majani kama kawaida yake amesimimia mdundo na masuala ya upishi zaidi na Fid kuspit rhymes zenye sumu kwenye mdundo wa Kinywele Kimoja.

Ngoma hiyo itakuwa ya tatu kutoka kwenye albam yake Kitaalojia baada ya Fid kutweet, “KitaaOLOJIA ‘ The completion of the trilogy ‘ 1-#ieLeweMitaa √ 2- #SihitajiMarafiki √ *next release lini? P_Majani anajua #Tuombeane Dua na Majani kujibu, “it’s my first song to mix this week, Video ASAP!!!! I can’t stop replaying that trak.”

Ommy Dimpoz kuachia single mpya wiki ijayo

Pamoja na kuwa na single mbili tu hewani, Nai Nai na Baadaye, Ommy Dimpoz anafahamika na wapenzi wengi wa muziki nchini na jirani ya Tanzania utadhani ana miaka zaidi ya kumi kwenye muziki. Na sasa wakati wengi wakiusubiria ujio wake wa tatu, leo msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Omary Faraji Nyembo ametangaza kuwa ataachia single yake ya mpya wiki ijayo.

Akiongea na Bongo5 Ommy amesema single hiyo imetengenezwa katika studio za THT ambapo producer ni Imma the Boy. Kuhusu jina la wimbo amesema anataka kufanya surprise lakini amesema wimbo huo unazungumzia malavidavi kama kawaida.