Wednesday, September 12, 2012

BABY MADAHA AONGEZA UKUBWA WA MATITI


KATIKA kusaka mvuto wa kimahaba, msanii wa filamu na muziki, Baby Madaha ameamua kuongeza ukubwa wa matiti yake (angalia picha).
Akipiga stori na Tollywood Newz, juzikati jijini Dar es Salaam, Baby alisema amefikia uamuzi huo kwa sababu wanaume huvutiwa zaidi na matiti na makalio makubwa.
“Najua Wabongo wanaweza kushangazwa na uamuzi wangu, lakini ni mambo ya kawaida kabisa kutafuta mvuto wa mahaba. Nimeanza na matiti, baadaye nitakwenda a makalio,” alisema.
Alipotakiwa kutaja hospitali aliyofanya upasuaji huo alijibu kwa kifipi: “Ni siri, siwezi kuitaja ila iko Nairobi (Kenya).”

WEMA ALIZWA TENA!



BEAUTIFUL Onyinye wa Bongo, Wema Isaac Sepetu, hivi karibuni alijikuta akipata wakati mgumu baada ya kukombwa vioo vya gari lake aina ya Toyota Mark X na vibaka wa Moshi, Kilimanjaro, Risasi Mchanganyiko lina habari kamili.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni ndani ya Viwanja vya Chuo cha Ushirika ambapo staa huyo alikuwa amehudhuria uzinduzi wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Akiwa katika burudani hizo, Wema ambaye muda mwingi alionekana kuwa mtu mwenye furaha ghafla alibadilika na kuishiwa na furaha alipolikuta gari lake likiwa limekongolewa vioo vyote vya pembeni.

Gazeti hili lilizungumza na Wema kuhusu tukio hilo ambaye alionekana kushangazwa na tukio hilo na kusema kuwa hakutarajia kukutana nalo kwa kuwa alikuwa akiwaheshimu sana watu wa Moshi.
“Imeniuma sana baada ya kukuta gari langu limekongolewa, wameiba vioo na ukiangalia nipo ugenini, halafu magari ni mengi yaliyokuwa yamepaki uwanjani, kwa nini yasiibiwe hayo mengine wakaiba langu tu, dah! imenikera sana,” alisema Wema kwa uchungu.
Hilo ni tukio lingine la Wema kulizwa, alishawahi kuibiwa nyumbani Sinza jijini Dar baada ya wezi kuruka ukuta na kumkomba baadhi ya vitu vya thamani, pia alishawahi kuibiwa vitu vingine ndani ya gari Uwanja wa Taifa.

JUMA NATURE NI BABA YANGU ILA AMENIKATAA



Kijana huyu anadai kuwa yeyey ni mtoto wa msanii Juma Nature na kujitambulisha kama Samson Juma Kassim Kiroboto, Samson anatokea Morogoro na kwa maelezo yake yeye amezaliwa mwana 1995.
"mama yangu ameshafariki na nilishawahi kwenda mpaka kwa baba yangu Juma Temeke nikiwa na bibi yangu, lakini aliponiona tu akanifukuza akasema hataki kuniona tena " hayo ndio yalikua maelezo ya Samson.
unaona kuna kufanana na nature katika picha hiyo?

Afisa mmoja wa ubalozi wa Marekani ameuawa na wengine wamejeruhiwa wakati kundi la watu waliojihami na silaha walipovamia jengo hilo mjini Benghazi.




Inaaminika kuwa watu hao walikuwa wanaandamana kulaani filamu mmoja iliotengenezwa nchini Marekani ambayo wanasema inamkejeli Mtume Mohammed.


Jengo hilo liliteketezwa kabisa na wandamanji hao waliokuwa na hasira.
Maandamano hayo yalichochea makabiliano kati ya vikosi vya serikali na kundi la wanamgambo maarufu kama Ansar al Sharia brigade, mjini Benghazi.


Msemaji wa serikali ya Marekani, amelaani kitendo hicho na ameongeza kuwa wanashirikiana na idara ya usalama nchini Libya kuimarisha usalama kwenye balozi zake.


Taarifa zinasema kuwa wakaazi wa mji mkuu Tripoli, wamekuwa wakishawishiwa kupitia ujumbe kwenye tovuti za kijamii wafanye maandamano lakini hakuna aliyejitokeza.


Sehemu ya filamu hiyo inasambazwa kupitia mtandao wa Youtube kwa lugha ya kiarabu.
Maandamano sawa na hayo pia yamefanyika mjini Cairo nchini Misri. Kundi lingine la watu limeingia kwenye ubalozi wa Marekani na kuteketeza bendera ya nchi hiyo.


Taarifa kutoka Cairo zinasema, maelfu ya Waislamu na Wakristo wameungana kulaani filamu hiyo. Hata hivyo hakuna aliyejeruhiwa kwenye maandamano hayo yaliofanyika Misri.

Ndugu zangu,

Wengi wameendelea kuitikia wito wa kumchangia mjane wa marehemu mwandishi Daud Mwangosi .
Imeanza pia kujitokeza michango ya kijumuiya. Ni jambo jema sana. Hata hivyo, ili kuepuka kuchanganya siasa kwenye suala hili la kijamii na la kibinadamu katika kumsaidia mjane wa marehemu, kama mratibu wa harambee hii, napendekeza kuanzia sasa wale wote watakaochangishana kijumuiya, hususan za kiitikadi, basi, michango yao iwakilishwe hapa kama michango ya kutoka Jumuiya za Watanzania, popote pale walipo hapa duniani.
Natumia fursa hii pia, kwa kutambua kuwa kuna jumuiya mbali mbali za Watanzania, na za marafiki wa Tanzania kwenye karibu kila kona ya dunia hii, kuwaomba wenyeviti wa jumuiya hizo kukusanya japo michango midogo kwa Wanajumuiya wenzao, iwe Watanzania au marafiki wa Tanzania, walio na utayari wa kuchangia hata kiasi kidogo tu cha pesa kwa mjane wa marehemu.
Michango hiyo inaweza kuwasilishwa kwangu kwa njia zifuatazo; M-Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money au NMB Mobile. Kwa namba 0754 678 252, 0712 95 61 31, 0788 111 765 (Kwa walio nje mnaweza kutuma kwa Western Union, jina la mpokeaji- Maggid Mjengwa, Tafadhali nijulishe kama utatuma kwa njia ya Western Union)
Natanguliza shukran,

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI AFIKISHWAMAHAKAMANI LEO IRINGA


Askari anayetuhumiwa kumuua Daudi Mwangosi leo amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya mkoa wa Iringa na kusomewa mashitakata yake. Huku akiwa chini ya ulinzi mkali ambao ulifanya wanahabari waliofika mahakamani kujitahid kupata picha kwa ugumu.

Akisoma mashtaka mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya Daines lymo mwendesha mashtaka ameeleza kuwa mtuhumiwa Pacificus Cleophase Simon (23

HABARI KAMILI ITAKUJIA HIVI PUNDE

Waandishi waandamana kulaani mauaji ya mwenzao


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi amepongeza waandishi wa habari walioandama jana Dar es Salaam kwa kuzingatia sheria.

Dk Nchimbi ambaye ‘alivamia’ Viwanja vya Jangwani jana ambako maandamano hayo ya kulaani mauaji ya mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi yaliishia, alisema waandishi hao walifuata utaratibu.

“Hivi ndivyo inavyotakiwa, kufuata sheria, kwani walitoa taarifa Polisi lakini hata walipoambiwa kwamba Mnazi Mmoja njia ni nyembamba hivyo wahamie Jangwani hawakusita na walifanya hivyo.

“Ni tofauti na watu wengine ambao wakiambiwa msipite huku hali hairuhusu hulazimisha na matokeo yake ni mtafaruku na Jeshi la Polisi,” alisema Nchimbi alipozungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Jangwani. Alitoa mwito kwa makamanda wa Polisi wa mikoa kukaa na wanahabari na kujadiliana ili wafanye kazi pamoja na kuondokana na migogoro ambayo haina ulazima.

Waziri Nchimbi ambaye alipata kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, alisema yote yaliyozungumzwa na wanahabari jana Jangwani kwa Serikali yatafanyiwa kazi bila kusita.

Wahariri na waandishi wa habari wakiwamo waliopata kufanya kazi katika vyombo vya habari, waliandamana kimyakimya kulaani mauaji ya Mwangosi yaliyotokea Iringa katika maandamano ya Chadema, siku 10 zilizopita.

Mwangosi ni mwandishi wa kwanza nchini kuuawa akiwa kazini na wa 38 mwaka huu na kufikisha idadi ya waandishi 46 waliouawa wakiwa kazini duniani kote.

Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida, Waziri Nchimbi ambaye awali alilakiwa na uongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na kupanda jukwaani alijikuta akizomewa na kutakiwa kuondoka eneo hilo.

Awali akiwa peke yake, baada ya kuegesha gari mbali na eneo la mkutano, Nchimbi alitembea hadi walikokuwa wanahabari hao na kupokewa kabla ya kukumbana na kadhia hiyo.

Waandishi wa habari walipoulizwa ni wangapi wanataka Waziri ahutubie, walikataa na kumtaka aondoke huku wakihoji alichofuata.

Lakini tofauti na Nchimbi, aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayeaminika kuwa kada na mwumini wa Chadema, Dk Azaveri Lwaitama, bila kualikwa alipewa fursa ya kuhutubia mkutano huo.

Maandamano hayo yalianzia Channel Ten na kuishia Jangwani huku washiriki wakiwa na mabango ya kulaani mauaji hayo na wengine wakiwa na mfano wa silaha na baadhi yao wanaoaminika ni waandishi wa Kampuni ya HaliHalisi inayochapisha magazeti ya MwanaHalisi (lililofungiwa) na Mseto, walionekana na mabango yakilaani kufungiwa kwa gazeti hilo.

Akizungumza katika Viwanja vya Jangwani, Katibu Mkuu wa TEF, Neville Meena alisema mauaji ya Mwangosi yanaonesha kuwa mazingira ya kufanyia kazi kwa wanahabari si salama.

Alisema wahariri na waandishi wa habari walikuwa na uwezo wa kufanya jambo kubwa kupitia kalamu na kamera zao zaidi ya maandamano, lakini waliamua kutumia njia ambayo wananchi wa kawaida wanaitumia kudai haki zao.

Alisema TEF ilianza kwa kutoa tamko la kulaani na kuunda tume ya watu watatu ambayo itafanya utafiti wa kihabari kuhusu tukio hilo, utakaotumika kupata maazimio ya wadau wa habari.

Tume hiyo imeundwa na mjumbe kutoka TEF, Baraza la Habari Tanzania (MCT) na kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini. Meena alitaka waandishi wa habari kuendelea kuhabarisha wananchi kwa kufuata misingi ya taaluma ya habari.

“Tuendelee kufanya kazi, bila vyombo vya habari hakuna kitu kitakachoendelea na ndiyo maana hata Rais akitaka kuhutubia wananchi kila mwezi haendi Jangwani bali anatumia vyombo vya habari kufikia Watanzania zaidi ya milioni 40.”

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari (UTPC), Jane Mihanji pamoja na kulaani mauaji hayo kwa nguvu zote, alitaka Polisi kutambua kuwa mwandishi anapokuwa kazini anatakiwa kuheshimiwa kwa kazi yake kama inavyofanywa kwa polisi akiwa kwenye sare. Mhariri Mtendaji wa Nipashe, Jesse Kwayu alisema:

“Kama Mwangosi angekufa kwa njia nyingine, kingekuwa kifo cha Mungu, lakini kwa kuwa ameuawa kikatili ndiyo maana tuko hapa.

“Damu yake ndiyo mwanzo wa kubadilisha mwenendo wa Jeshi la Polisi nchini, wajue kuwa kodi za wananchi kama sisi ndizo zinazolipa mishahara, kuwanunulia magwanda kwa kazi ya kulinda raia na si kuua.”

Dk Lwaitama aliyetambulishwa kama rafiki wa wanahabari, alitaka waandishi kutochukia polisi wa ngazi ya chini na badala yake wachukie wanasiasa wanaowatuma na kuwatumbukiza katika siasa. Mwakilishi wa Africa Media Group, Dina Chahali alishukuru wanahabari kwa umoja wao wa kulaani mauaji ya Mwangosi na kuwa huo ndio mwanzo wa kudai haki ya habari na wanahabari.

Meena alipoulizwa baadaye na gazeti hili iweje Dk Nchimbi azuiwe kushiriki na Dk Lwaitama aruhusiwe, alisema hakuna aliyealikwa kwenye maandamano hayo zaidi ya waandishi wa habari na Dk Lwaitama alikuja kama wananchi wengine walivyojitokeza.

“Dk Lwaitama hakupata mwaliko, ila penye watu wengi panakuwa na mengi kama unavyojua ... sisi wenyewe tunashangaa, ni kupitiwa tu ila naye hakupewa mwaliko,” alisema bila kufafanua kama wananchi wengine nao walikuwa na haki ya kupanda jukwaani kuhutubia wanahabari.

Arusha Mkoani Arusha, polisi walifika eneo la Jengo la CCM la Mkoa, kuzuia maandamano ya waandishi waliokuwa wamejikusanya wakiwa na mabango yao, yenye ujumbe mbalimbali wa kulaani mauaji ya Mwangosi.

Polisi walieleza kuwa wanakabiliwa na uhaba wa askari wa kulinda maandamano hayo, kwa sababu ya ugeni mkubwa wa Mkutano wa Mazingira. Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC), Eliya Mbonea aliwaomba waandishi kutii amri ya Polisi, huku akiwasomea taarifa ya Jeshi hilo iliyotolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD), Lotson Mponjoli ya kuzuia maandamano hayo.

'Serikali isiiogope Malawi'


SERIKALI imetakiwa kuwa makini katika kushughulikia mgogoro uliopo na Malawi kuhusu mpaka ndani ya Ziwa Nyasa na kutokubali kuliachia ziwa hilo kutokana na umuhimu wake kwa uchumi.

Akizungumza katika kikao kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na wazee wa Mji Mdogo wa Lituhi wilayani Nyasa, mmoja wa wazee hao, Conrad Chale alisema, Serikali haipaswi kuogopa wala kuliachia Ziwa Nyasa kwani mpaka uko ndani ya ziwa na si nje kama Malawi inavyodai.

Alisema madai hayo ya Wamalawi hayana msingi wala ukweli wowote kwani kabla na baada ya nchi hiyo kupata uhuru, karibu huduma zote za muhimu walikuwa wakipata Tanzania na kuishi nao kama ndugu moja huku wakitambua uwepo wa mpaka katikati ya ziwa.

Chale alisema Wamalawi ndiyo wanaotakiwa kuilipa Tanzania baada ya kupata huduma nyingi za kijamii kutoka nchini hasa wale wanaoishi kando kando ya ziwa ilo.

Alisema Serikali ya Malawi haipaswi kung’ang’ania kuwa ziwa hilo ni lake kwani upo ushahidi wa kutosha unaoonesha uwepo kwa mpaka wa nchi hizo mbili katikati ya ziwa na kusisitiza umuhimu wa kuheshimu mpaka huo ili kuepusha nchi hizo kuingia vitani na kusababisha madhara kwa wananchi.

Aliiomba serikali, kulinda mpaka huo kwa gharama ikiwemo rasilimali zilizopo katika ziwa hilo ambalo ndiyo tegemeo pekee la uchumi kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa.

Waziri Membe alisema Serikali itaendelea kutafuta muafaka wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania ndiyo maana imekwenda kwa wazee waliokuwepo katika maeneo hayo kwa muda mrefu, ili kupata ushahidi kuhusu madai ya nchi ya Malawi.

Waziri Membe ambaye aliongoza ujumbe wa wataalamu mbalimbali katika ziara hiyo, aliwataka wananchi kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali na kutokuwa na wasi wasi kwani tatizo hilo linashughulikiwa na ikibidi watafika hadi mahakama ya kimataifa kutafuta haki ya Watanzania.

Alisema Malawi wanatafuta sifa mbele ya jumuiya ya kimataifa, lakini haitafanikiwa kwani wanafahamu ukweli juu ya mpaka huo na uhalali wa Serikali ya Tanzania kumiliki sehemu ya Ziwa Nyasa.

Aliwashukuru wazee wa wilaya hiyo kwa kuunga mkono juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali katika kutafuta namna ya kumaliza mgogoro huo na uwepo wa wazee hao ambao umesaidia kupata ukweli.

Wakati huohuo, Serikali imeombwa kuboresha huduma mbali mbali za jamii kwa wananchi waishio kando ya ziwa Nyasa, ili kupunguza kero kubwa za muda mrefu zinazowakabili wananchi hao zinazosababishwa na ukosefu wa miundombinu.

Akitoa kilio chao mbele ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, mmoja wa wakazi wa Liuli, Raphael Kambanga alisema kukosekana kwa miundombinu ya kisasa ni moja ya sababu zilizoifanya Wilaya ya Nyasa kubaki masikini licha ya kuwepo kwa rasilimali za kutosha.

Kambanga alimueleza Waziri Membe kuwa hivi sasa bidhaa nyingi zinazotumiwa na wananchi wa Nyasa zinatoka Malawi na Msumbiji jambo ambalo ni hatari kwa uchumi.

Alifafanua kuwa uhusiano huo wa kibiashara na nchi jirani, unaikosesha Serikali mapato ya kutosha kutokana na kodi za kuingiza bidhaa huku wafanyabiashara wajanja wakitumia mwanya huo kufanya biashara za magendo.

Alisema wanalazimika kutumia muda mwingi kufuata huduma za jamii mbali huku muda wa kufanya shughuli za maendeleo ukipita, kitu ambacho ni hatari kubwa kwa kuwa wanashindwa kufanya kazi zinazoweza kupunguza umasikini katika familia zao.

"Tunakuomba pamoja na matatizo tuliyonayo kati yetu na Malawi, mtukumbuke sisi tunaoishi huku pembezoni… hali yetu ni mbaya ndiyo maana hata wenzetu Wamalawi wanatumia nafasi hiyo kuhalalishia mpaka nje ya ziwa kutokana na ukimya wa Serikali yetu," alisema.

Kambanga aliitahadharisha Serikali juu ya mipaka iliyopo ambayo hakuna ulinzi wa kutosha na inaweza kutumika kwa kupita maadui hasa kutoka Malawi na Msumbiji kufanya lolote wanaloweza kwa maslahi ya nchi zao, kwa hiyo ni vizuri serikali kuangalia maeneo hayo mara kwa mara.