MSANII wa Hip Hop nchini Kenya anayejulikana kwa jina la Prezzo amejikuta akizalirishwa kwa kupewa maneno makali ya kumchafua ikiwemo kuitwa 'serengeti boy' na binti wa kichaga kutoka nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Starlisha Tillya 'Chagga Barbie' kutokana na sababu za kimapenzi.
Inasemekana wawili hao walikuwa na mahusiano ya kimapenzi yaliyoanza kushamili kwa kasi mwaka jana huku kila mmoja wao kuonekana kufurahia kuwa pamoja kabla ya mahusiano hayo kuingiwa na doa lililoibua utata.
Chagga Barbie ameutumia ukurasa wake wa Istagram kuanika hasira zake kwa kutuma message za siri walizokuwa wakitumiana wakati mapenzi yao yakiwa motomoto.
"Y nimeposti baadhi ya chati ni kwa sababu umeanza kwa kushare kwa dada zako sasa nitarusha voice note watu wakusikie live ulivyokuwa hautumii akili, mwanaume timamu hafanyi mambo hayo , eti hapa ulikuwaukijibabishaaaa loi unajua hapa nilipokuangalia ndipo nilianza kustuka nikasema huyu babu mwenye rangi za blonde kaa mie nafanya nae nini?" aliandika Chaggga kwenye ukurasa wake huo.
Mbali na hilo pia mwanadada huyo aliziweka wazi baadhi ya message walizokuwa wakitumia ambapo moja ya message hizo zilionesha walikuwa wakimjadili mwanamuziki maarufu nchini Tanzania Diamond Platnum.
Ambapo ilishawahi kuripotiwa kuwa na hali ya kutoelewa kwa wasanii hao wawili mwaka jana bila ya kuweka wazi chanzo cha ugomvi wao ni nini.
Licha ya kuwepo kwa marumbano hayo kwenye mtandao huo huku kwa upande wa msanii huyo Presso aliandika maneno machache kwenye ukurasa wake huo, bado haijawekwa wazi kisa cha ugomvi huo na marumbano ya udharilishaji.
No comments:
Post a Comment