Tuesday, January 29, 2013

Picha: Timbulo na Rose Ndauka waigiza filamu iitwayo “World of Benefit”




Msanii mahiri wa muziki wa Bongofleva nchini, Ally Timbulo, ameanza safari mpya kwenye tasnia ya filamu kwa kushoot filamu na Rose Ndauka akiwa kama ni mhusika mkuu. Filamu hiyo inaitwa World of Benefit.

Ndani ya filamu hiyo Timbulo anakuwa ni kijana anaye onyesha mapenzi ya kweli kwa Rose aliyeolewa. Waigizaji wengine kwenye filamu hiyo ni pamoja na Mohamed Olutu ‘Mzee Chilo’, Mama Mjata, Hemed Suleiman ‘Phd’, na Awadhi Saleh muigizaji anayekuja juu katika tasnia ya filamu nchini.

“Nimepata bahati kufanya kazi na wasanii wakongwe kwahiyo ni kitu cha kujivunia na pia mimi ni mhusika mkuu kwenye hii filamu ambapo Rose Ndauka kaolewa katika ndoa ya mke zaidi ya mmoja. Rose yupo nyumba ndogo kwahiyo nyumba aliyopewa na bwana wake ananiita niishi naye kwakuwa mimi ni mpenzi wake wa muda mrefu kwahiyo namwonyesha “True Love” na tunapendana sana na yule bwana wake tunamfanya kama mwezeshaji wa maisha yetu” anasema Timbulo.

Rose-Ndauka-Timbulo-Ali

Seleman-mkangara-Mapunda-Selles

Filamu ya World of Benefit imetayarishwa na mtayarishaji wa filamu Hamees Suba ‘Kemikali’ na inaongozwa na Selles Mapunda ‘Director of Directors’, akisaidiwa na Suleiman Mkangara ‘Striker’ kwa upande wa upigaji picha wapo wataalamu kutoka Bollywood chini ya kampuni ya Pilipili Entertainment ya jijini Dar es Salaam.

Picha: Filamu Central

No comments:

Post a Comment