Wednesday, February 6, 2013

Polisi walioitwa kumsaidia Jaydee wamgeuka, waita waandishi wa habari wapate habar




Jana kupitia mtandao wa Twitter mwanadada Lady Jaydee alisimulia kitendo kilimchokera baada ya polisi walioitwa kwenda kumsaidia akiwa kwenye chumba cha hoteli baada ya kuzidiwa ambao waliamua kuwapigia simu waandishi wa habari za udaku waje wapate picha na habari.

“Police mnatumwa kuja kuni rescue mgonjwa Hotel Room, mnaita waandishi waje kuchukua story! Hamjanitendea haki, nimesikitishwa,” alitweet Jaydee.

“Nawaambia I can’t walk wananilazimisha shuka watu watakubeba gari tumepaki nyuma. Kumbe camera ziko chini huko zinangoja.”

Akijibu swaliu la Bongo5 lililouliza kama waandishi hao walipata walichokitaka Jaydee alijibu, “I told them walete doctor humo hotel room kama hawaezi waondoke. Hotel staff told me nsishuke kuna camera chini.”

“Mwenyewe nashangaa hawakuwa wanajali mimi kupata nafuu bali maslahi. Hakuna utu hapo.”

Alimalizia kwa kuandika, “Hamtujali, na hamjali lolote. Kila mtu ana shida zake ila msichukulie advantage kutunyima haki zetu za msingi. Nimeumia sana!

Hata hivyo Jaydeea alidai kuwa kwa sasa anaendelea vizuri ingawa hatukuweza kufahamu alikuwa hoteli gani na wapi pamoja na tatizo lililokuwa likimsumbua.

Pole Jide.

Tuesday, February 5, 2013

Zola D kuanzisha kipindi cha TV cha mazoezi!



Hivi karibuni Bongo5 ilichat na rapper na bondia nchini Tanzania, Zola D ambaye alisema ana mpango wa kuanzisha kipindi cha TV.

“Now nina mpango wakuanzisha kipindi cha TV pia na kurusha video zangu za mazoezi kwenye Youtube ili kila mtu alie nyumbani aweze kufanya mazoezi sio mpaka uingie gym, “ alisema Zola.

“Mimi siendi gym kufanya mazoezi nafanya home pia gym naenda kama nina game ya boxing,ili niweze kufundishwa na mwalimu mbinu mbali mbali za mapigano na ushindi.”
Zola akiwa na P-Funk

Akijibu swali la ni vipi ameweza kuujenga mwili wake kiasi hicho, Zola amesema, “Mwili wangu nimeujenga toka miaka mingi sana sasa nina miaka 18 tokea nimeanza kufanya mazoezi ndio maana unaweza kuona mwili wangu umejengeka sana kuliko watu wengine hapa Bongo. Pia mazoezi ninayofanya ni mazoezi ya mapigano na mazoezi ya kujenga nguvu kama push up kukimbia,kuruka kamba,na kufanya swimming sababu napenda sana mazoezi na ndio starehe yangu kubwa,pia nafanya mazoezi kila siku ndio chakula cha maisha yangu,so kila siku nazidi kugain na kuongezeka.”

“Mazoezi yananisaidia sana kwenye afya yangu coz sijaumwa malaria huu ni mwaka wa 4 pia mafua kifua nk,coz ukifanya mazoezi damu inakuwa na nguvu sana,”aliongeza.

Hata hivyo Zola amesema hana pambano lolote hivi karibuni na kuongeza kuwa mchezo wa ndondi kwa Tanzania haulipi.

“Game za Bongo hakuna pesa kabisa ni kuumizana tu promoter wenyewe njaa tu, promoter hana hata baiskeli. Nia yangu ni kupigana ngumi za nje na kuitangaza Tanzania.Nipo tayari kupigana na bondia yoyote mkubwa wa dunia coz najua nina kipaji cha sports pia napenda sana kupigana nikitoka damu ndio naskia raha sana najiona mimi ndio mwanaume.”
Zola na Mad Ice


Kuhusu kuzichapa kiukweli na Mad Ice ambaye pia ni bondia na ameigiza kwenye video yake ya Knock OUT, Zola amesema Ice ni mtoto mdogo.

“Mad ice hawezi kupigana na mimi,pia mimi ni mwalimu wake namfundisha boxing. Nawaomba watanzania wazidi kuniombea dua niweze kutimiza ndoto zangu za kupigana level za kimataifa,muziki wangu level za kimataifa na michezo yangu mingine kama kukimbia mita 100, mita 200,kuruka viunzi,kucheza rugby, kupigana boxing mixed martial arts.”

Video ya Me & You ya Ommy Dimpoz ft. Vanessa Mdee kuzinduliwa Feb 10, Maisha Club



Jumapili hii ya February 10, Omary Nyembo aka Ommy Dimpoz ataizindua rasmi video ya wimbo wake Me and You aliomshirikisha Vanessa Mdee. Video hiyo imefanywa na Ogopa Dj’s wa nchini Kenya.

Katika uzinduzi huo utakaofanyika New Maisha Club, Ommy atasindikizwa na wasanii wenzake wakiwemo Diamond,Dully Sykes,MwanaFA na performance kutoka kwa wasanii wakali wa Africa Mashariki.

Prezzo na Goldie kufunga ndoa February 9



Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali nchini Nigeria, rapper Jackson Makini aka Prezzo anatarajia kufunga ndoa na mwanamuziki wa Nigeria Goldie February 9.

Habari hiyo pia imeandikwa na website ya Big Brother Africa. Harusi hiyo itafanyika jijini Lagos, Nigeria.

Katika hatua nyingine mwakilishi wa mwaka jana wa Nigeria kwenye shindano la Big Brother Africa, anatarajia kuanzisha Reality TV show yake.Goldie anaanzisha show hiyo iitwayo ‘Tru Friendship’. ‘Tru Friendship’ itaonesha maisha ya kila siku ya muimbaji huyo wa Skibobo, Goldie, yote kama mtu maarufu na kama Susan Harvey.

Show hiyo itaanza kuonekana mwishoni mwa mwe

Mwasiti afunguka kuhusiana na mali anazomiliki!!


Hitmaker wa Nalivua Pendo na Mapito, Mwasiti Almas ameelezea mafanikio aliyoyapata kupitia kazi yake ya muziki ambapo amefanikiwa kununua gari lenye thamani ya milioni 16 na mjengo anaoumalizia maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Kupitia kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Mwasiti alisema nyumba hiyo yenye vyumba vitano inatarajiwa kumalizika baada ya miezi michache ijayo.

Monday, February 4, 2013

Wafuasi Chadema, CCM wagombea mti wa bender




SHEREHE za miaka 36 za kuzaliwa kwa CCM jana ziliingia dosari, baada ya kuibuka vurugu kubwa kati ya wafuasi wa chama hicho na Chadema mkoani Dodoma wakati wakigombea eneo na mti wa kutundika bendera za vyama vyao.

Vurugu hizo zilizotulizwa na Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU), zilitokea jana mchana katika uwanja huo uliopo karibu na Baa ya Mwanga, baada ya CCM kung’oa bendera ya Chadema iliyokuwepo uwanjani hapo, ili waweke bendera zao kwa ajili ya mkutano ambao ulikuwa sehemu ya maadhimisho hayo.

Vurugu zilizuka baada ya wafuasi wa Chadema kuwataka wenzao wa CCM waendelee na mkutano katika eneo hilo kwa sharti la kurejeshwa kwa bendera iliyong’olewa. Wafuasi wa vyama hivyo wakiwamo wabunge wa CCM walionekana wakivutana kunyang’anyana mti wa bendera.

“Baada ya CCM kugoma, Chadema walijaribu kurudisha bendera hiyo kwa nguvu, jambo ambalo lilifanya wafuasi wa CCM waanze kuokota mawe na kuwarushia wapinzani wao hao, huku Chadema nao walianza kujibu mapigo,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Baadhi ya wabunge wa CCM walioshiriki katika vurugu hizo na majimbo yao kwenye mabano ni Ismail Aden Rage (Tabora Mjini), Nyambari Nyangwine (Tarime), Seleman Jafo (Kisarawe), Said Mtanda (Mchinga) na Mary Chatanda (Viti Maalumu).

Baadhi ya wafuasi wa CCM walionekana wakibeba mawe na kuwapiga wenzao wa Chadema na kusababisha tafrani kubwa katika eneo hilo la mkutano.

Katibu wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, Jellah Mambo alisema kuwa tukio hilo limetokana na wafuasi wa CCM kung’oa bendera ya Chadema iliyokuwa ikipepea eneo la Mwanga Baa kulikofanyika sherehe za chama chao (CCM).

“Kwanza wamechukua bendera yetu. Halafu tumeshangazwa na CCM kuruhusiwa kufanya maadhimisho yao wakati kuna agizo la Mkuu wa Mkoa na polisi kukataza mikusanyiko ya kisiasa wakati wa Bunge.

“Kwa nini sisi (Chadema) tuzuiwe mikutano yetu wakati wenzetu wanafanya? Huku si kutenda haki....Tulikuwa na mikutano ya kuimarisha chama katika kata kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, lakini tumezuiwa na tukaheshimu mamlaka,” alisema katibu huyo.

Pia tulikuwa tufanye mkutano na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, lakini tukazuiwa na tuliheshimu amri hiyo, alisema.

Mambo alisema katika vurugu hizo wafuasi wawili wa Chadema; Idd Kizota na Anord Swai waliumizwa na kushonwa nyuzi saba usoni.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Ezekiel Mpuya alisema hana taarifa za majeruhi hao.

“Ni vigumu kujua, unless (isipokuwa) wafike hospitalini wakisindikizwa na kundi la wafuasi wenzao waliokuwa kwenye sare. Kama walikuja kama wagonjwa wengine sio rahisi sana kwangu kujua,” alisema Dk Mpuya.

Kumi mbaroni

Vurugu hizo zilizosababisha watu wawili kuumizwa vibaya, zililazimisha Jeshi la Polisi kuwatia mbaroni watu kumi wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa Chadema

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alikiri kutokea vurugu hizo, lakini akasema bado anafanyia kazi suala hilo.

Kamanda Misime alikiri Serikali mkoani Dodoma kuzuia mikutano ya kisiasa wakati wa Bunge, lakini akasema kwa CCM ni tofauti kwa kuwa hizo ni sherehe zao za kuzaliwa kwa chama.

“Ninasoma hapa magazeti yenu, mmeandika wenyewe maadhimisho ya miaka 36. Sasa hawa wanaadhimisha hiyo miaka 36 na siyo mkutano wa kisiasa...Tulichokataza ni maandamano, misafara ya pikipiki na kufanya mikutano ya siasa,” alisema Misime.

Akihutubia katika mkutano huo baada ya hali kutulia mgeni rasmi, Mbunge wa Jimbo la Tarime, Nyangwine aliwakandia wapinzani na kusema kuwa wanachokifanya ni kuendeleza vurugu nchini na hawana sera ya maendeleo.

“Hivi jamani, hii leo hawa jamaa watasema nini? Kama suala la barabara, leo hii unaweza kutoka Mtwara hadi Mwanza kwa baiskeli, kama maji, michakato inafanyika, kama umeme ndiyo usiseme, hivi wanataka nini?

“Hawa jamaa wamezoea kufanya vurugu...Si mmeona wenyewe hapa, hawana lolote zaidi ya kufikiria vuru, wananchi msikubali kuhadaiwa,”alisema.

JK akemea mifarakano

Akizungumza mkoani Kigoma kulikofanyika maadhimisho hayo kitaifa, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alikemea siasa za makundi ndani ya chama, akisema tabia hiyo haijengi.

“Mifarakano ndani ya chama inayopaliliwa na viongozi ndani ya chama, inakibomoa chama na ndiyo maana tumepoteza majimbo matano katika uchaguzi uliopita,” alisema.

Aliendelea:“Ninasoneneka sana kuona viongozi wetu wanajiingiza katika makundi, tabia hii haijengi, turejee katika maazimio yaliyopitishwa katika mkutano mkuu uliopita, ambayo yalisisitiza kuwapo kwa umoja na mshikamano.”

Rais Kikwete alisema angetamani umoja na mshikamano wa chama hicho ungeendelea kudumu, ili amalize muda wake akikiacha chama kikiwa imara na kuendelea kushika dola.

“Mimi sasa ninaelekea kwenye ungwe ya mwisho ya uongozi, nataka nikabidhi kijiti kwa mwana-CCM…Nataka niondoke nikiwa nimeicha CCM imara “ alisema Rais Kikwete .

Katika hotuba hiyo Rais Kikwete pia aligusia maendeleo yaliyofikiwa katika kipindi cha utawala wake akitaja maeneo kama ujenzi wa barabara, madaraja na uimarishaji sekta ya maji kuwa ni baadhi ya maeneo yaliyopiga hatua.

Alisema atapondoka madarakani jambo kubwa ambalo angependa Watanzania wakumbukuke kwalo ni kuitwa bwana maendeleo na hivyo sasa anaendelea kuisimamia vyema ilani ya chama chake ili kuendelea kukamilisha miradi iliyobaki.

Mapema Rais Kikwete aliongoza mamia ya wakazi wa Mji wa Kigoma katika matembezi ya mshikamano ikiwa ni ishara ya kuhimiza umoja na mshikamano kwa Watanzania.

Kikwete aliungana na viongozi wenzake Makamu Mwenyekiti CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana, lakini katika hali isiyo ya kawaida baadhi ya viongozi wa chama hicho hawakushiriki, akiwemo wenyeviti wastaafu, Benjamin Mkapa na Ali Hassan Mwinyi.

Wengine ambao hawakuwepo katika matembezi hayo ni pamoja na makatibu wakuu wa zamani; Yusuph Makamba na Willison Mukama na wajumbe wote wa sekretarieti ya chama hicho iliyoteuliwa Novemba mwaka jana.

Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na viongozi wa vyama vya siasa vya PPRD cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kile cha CNDD-FDD ambavyo vilisindikizwa na vikundi vya sanaa kutoka katika nchi hizo jirani.

NEW VIDEO:- WAKALI WA MEDIA Tzee -KIDOLE KWA MACHO





A BRAND NEW VIDEO FROM MINOR CODE 324000

[KIDOLE KWA MACHO by WAKALI WA MEDIA Tzee]

{"Young Jimmy, Ander Guy, Supri Sudi, William Fuko, Sulenga B Boii, Ally Stilly, Kibeby Kimbe, Mubaraq Jembe and Curtis Mashaka''}

Producer; JIMMY JIZZE,
Studio; ROCCANA BASEMENT
VIDEO Directed by Emmanuel (Minor Code 324000)