Thursday, October 11, 2012

DIAMOND PLATNUMZ APIGA KAMPENI NGORONGORO CRATER

Diamond Platnam'z

SANII wa muziki wa kizazi kipya,Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewataka watanzania kulipigia kura bonde la Ngorongoro kuwa moja ya maajabu saba ya Afrika na pia kujenga tabia ya kutembelea vivutio vya utalii vya ndani.
Akizungumza mjini Ngorongoro, Diamond ambaye alikuwa huko kujionea bonde hilo ambalo ni la kipekee ulimwenguni, amesema hakuwahi kufikiria kwamba kuna sehemu nzuri ambayo hata watanzania wanaweza kwenda kutembea na kujionea vivutio vilivyopo.
“Hii ni mara yangu ya kwanza kufika hapa, lakini kwa kweli nimeshangazwa na jinsi palivyo pazuri, wanyama, mito ambayo inapita huku chini, mi huwa naona kwenye televisheni tu katika kile kipindi cha National Geography cha DSTV lakini sikujua kama mambo haya yapo kweli kwetu.
“Nawaomba watanzania wenzangu waweze kutembelea Ngorongoro na vivutio vyetu vya utalii kwa sababu kuna mengi ya kujifunza, leo kama isingekuwa Afrika sidhani kama kungekuwa na kipindi kama National Geography, na gharama za kuja huku si kubwa, hatupaswi kuogopa, hivi ni vitu ambavyo vinawezekana kabisa suala ni kujipanga,” amesema.
Amesema wenzetu kutoka Ulaya wamekuwa wakijipanga kuweza kutembelea sehemu Fulani jam bo ambalo linawafanya waweze kutembelea nchi nyingi kufanya utalii.
“Pamoja na kuja kupunguza mawazo lakini sehemu kama hii inasaidia kuelemisha, mwito wangu kwa watanzania wenzangu, mashule hata vyuo waweze kuja hapa, inakuwa rahisi zaidi kumfundisha mtoto kuhusu Simba, Twiga, au bonde la Ngorongoro kwa kumuonyesha hiki kiko hivi, nadhani kama watoto watakuwa wanasoma kwa vitendo hawawezi kushindwa mitihani yao kwa sababu kumbukumbu inabaki kichwani kwa kile walichokiona,” amesema.
Msanii huyo alikwenda Ngorongoro baada ya kumalizika kwa tamasha la Fiesta ambapo alikuwa mmoja wasanii waliofanya vizuri. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ilimualika Diamond huko. Ngorongoro ni moja kati ya vivutio vya Tanzania vinavyotakiwa kupigiwa kuingia katika maajabu saba ya Afrika
Diamond plutnim'z

No comments:

Post a Comment