Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbass Kandolo
Mkuu wa mkoa wa mbeya Abass kandolo amevunja baraza la
madiwani wilaya ya rungwe mkoa wa mbeya na kutanganza rasmi halmashauri ya
rungwe itakayo kuwa na kata 26 na kuitangaza halmashauri ya busokelo
itakayokuwa na kata kumi na moja.
Akiongea na baraza la madiwani mkuu wa mkoa wa mbeya amsema
kuwa serikali imeanzisha kifungu (sub_vote) na>7813140 na kutenga fedha
kwenye bajet ya mwaka wa fedha 2012/2013 kwa ajili ya halmashauri ya busokelo,
yenye jumla ya tsh 12,549,250,889/=
Halmashauri ya rungwe itakuwa ikiongozwa na mkurugenzi noel
mahyenga pia halmashauri ya busokelo itakuwa inaongozwa na imelda ishuza
aliyeteuliwa kuiongoza halmashauri ya busokelo inayoanza leo kuwahudumia
wananchi wa busokelo.
Akitoa saram za mkoa mkuu wa mkoa wa mbeya kandolo amewataka
wananchi kufanya kazi kwa bidii na kuchangia shughuri za maendeleo na hili
itazizifanya halmashauri kuwa maendeleo zaidi.
Pia amesema haitakuwa na maana kuwa na halmasahauri mbili
bila ya kujibidisha kufanya kazi za maendeleo na kukusanya ushuru ili
kujiwezesha kujitegemea
Zaidi amewapongeza wananchi wa busokelo kupata huduma za
maendeleo karibu na wao
Amewahakikishia kuwa serikali kwa kuzingatia ahadi ya rais
wa jamuhuri ya muungano wa tanzania dr jakaya kikwete aliyoitoa katika kipindi
cha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ombi lililotolewa na mbunge wa
rungwe masharika prof mark mwandosya katika kiwanja cha tandale na rais
aliahidi kuifanya wilaya ya rungwe kuwa na halmashauri mbili rungwe na busokelo
na leo ahadi hiyo imetimia kwa kupata halmashauri ya mpya ya busokelo.
Baraza la Madiwani kabla ya kuvunjwa
MKUU WA WILAYA RUNGWE CYPRIAN MEELA AKIONGEA NA MADIWANI
KABLA BARAZA LA MADIWANI HALIJAVUNJWA
No comments:
Post a Comment