Tuesday, October 30, 2012

Sumalee azungumza jinsi Land Cruiser VX yake ilivyoibiwa


Huenda ukawa unaisoma habari hii kwa mara ya kwanza. Story ni kuwa wajanja wameiiba gari ya Sumalee aina ya Land Cruiser VX katika fukwe za Coco Beach jijini Dar es Salaam alikokuwa ameenda kula upepo.

Kupitia XXL ya Clouds FM, hivi ndivyo alivyosimulia tukio hilo:

“Nilikuwa Coco nimepaki nikatoka si unajua mambo yetu, na siyo kama walivunja wamefanya kuchukua tu yaani kama gari yao hata mimi sielewi ilikuaje. Mimi ninawaambia hiyo wamechukua, ni gari niliyoipata kwaajili ya Hakunaga, nitaimba nyimbo nyingine zaidi ya Hakunaga na mimi hiyo gari nitaipata kwasababu mimi ni wa hapahapa mjini,wafanye mengine siyo hiyo tu,ni ujinga tu,watalipeleka wapi hilo gari, spare za used zote niko nazo Kariakoo,hakuna mtu yoyote atakayelitaka wala kulinunua watu wanalijua,mwenyewe mimi maskini ,nimejichanga mwenyewe nimechukua gari sio kama nina hela, hiyo gari nilikuwa na uwezo hata wa kujenga nyumba ila nikaamua ninunue gari imeniuma sana.”

No comments:

Post a Comment