Taarifa hiyo imetolewa na kaimu meneja mawasiliano wa
mamlaka ya mawasiliano (TCRA) Semu Mwakyanjala ambaye amesema mamlaka hiyo
itaanza kwa kutoa elimu kwa umma kuhusiana na umuhimu wa kununua simu halali.
Ameliambia gazeti la Daily News Jumapili kuwa hatua hiyo
itachukuliwa na nchi zote wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki zikiwemo Rwanda , Uganda
na Burundi .
Kuna taarifa kuwa makampuni mengi ya simu nchini Tanzania
yameupokea mpango huo kwa shingo upande kwa hofu kuwa yatapoteza wateja wengi.
Kwa upande wa tume ya mawasiliano ya Uganda (UCC) hatua hiyo
ya kuzima simu bandia itafanyika mwishoni mwa mwezi November.
No comments:
Post a Comment