Friday, October 19, 2012

Waliyoandika mastaa kuhusiana na vurugu za Dar


Kwa zaidi ya saa nne mada kwenye mitandao ya kijamii kuanzia mchana ilikuwa ni hali ya vurugu iliyokuwa ikiendelea katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam baada ya waislam kufanya maandamano katika maeneo hayo. Vurugu kubwa zimetokea katika maeneo ya Kariakoo, Magomeni, Mtambani – Kinondoni na kwingine. Polisi wametumia mabomu kuwatawanja waandamanaji hao na saa hali sasa ni shwari.




Haya ni baadhi ya maoni ya watu maarufu nchini kuhusiana na vurugu hizo.

ESTHER WASIRA

Mwalimu Nyerere must be MOURNING in his grave! Nani ameharibu Amani ya nchi yetu!! Leo ‘Bandari ya Salama’ ndio huu uwanja wa damu???!!! Tunachinjana kama wanyama!! Oh Mwalimu,ndio haya uliyotuelekeza!? Nani alaumiwe?? Hii dhamana ni ya nani?? Oh Heavenly Father,pour out your wrath on all who destroy our long-lived Peace!!

Maria Sarungi-Tsehai

Inabidi sote tutake amani na tuhakikisha tunakuwa na amani. Mi naamini watanzania tulio wengi tunapenda amani ila tatizo kuna presha nyingi za kisiasa, kiuchumi na kijamii kutupotosha. Tusimame pamoja.

Lady JayDee

Kumbe Tanzania kuna udini?

Soggy Doggy

TANZANIA…SHETANI GANI TENA HILI LIMETUKUMBA??????

GODZILLA

“We must learn to live together asbrothers, or we are going to perish together as fools.”

Albino Fulani

Hivi unafikiri JK angesimama akasema, “Waislam mnaoleta fujo,mimi siko na nyinyi” fujo zingeendelea?They know what house they are knocking!

No comments:

Post a Comment