Msanii wa kike wa nchini Kenya, Avril ameamua kuonesha kuwa biashara ya headphones inaweza kufanywa na msichana pia kwa kuanzisha aina ya ear/headphones zake ambazo kama zikiwa na ubora mzuri huenda kwenye soko la Afrika Mashariki zikatoa upinzani kwa zile za Dr Dre Beats By Dre.
Hata hivyo mradi wake huo utapewa shavu na wizara ya elimu ya juu, sayansi na teknolojia ya nchini Kenya.
Ear phones hizo zitajulikana kama Gs N Fs na zitakuwa sehemu ya mradi wa kuwainua vijana wenye vipaji na mawazo kuhusiana na teknolojia ambao hawana rasilimali za kuendeleza vipaji vyao.
No comments:
Post a Comment