Saturday, November 24, 2012

Chezea Tuzo; AY Ampiku Diamond Kufanya Kolabo Na J Martins



Kwa wale ambao walikuwa wakifuatilia kwa karibu, habari za msanii Diamond kwa kipindi kirefu cha mwaka huu watapata kushangaa nini kimetokea kwa kolabo yake na msanii J Martins ambayo amekuwa akiitangaza mara kwa mara huko nyuma.


Well kwa sasa inaonekana msanii huyo kutoka Nigeria atafanya kazi na msanii aliyepata tuzo ya video bora Afrika Mashariki kupitia Kolabo na wasanii wa Kenya Sauti Sol, Ay na swahiba wake wa karibu Mwana FA.
Kwa mujibu wa tetesi za chinichini, mipango yote ya kolabo hiyo imeshaiva na pengine kazi hiyo ikakamilika siku si nyingi.
Well tusubiri na tuone yatakayojiri.

No comments:

Post a Comment