Thursday, November 22, 2012

Ni Mikosi Mfululizo Kwa Msanii Barnaba



Msanii Barnaba Elias ambaye anajulikana kwa sasa kama Baba Steve amekumbwa na maswahibu mfululizo ambayo itambidi kuwa makini la sivyo na yeye ataingia kwenye vitabu vya wasanii ambao wanakumbwa na mikasa inayoweza kumpelekea kukosa mwelekeo wa kimuziki.

Kwa mujibu wa habari ambazo zipo kitaani msanii huyo alikumbwa na mkasa wa kwanza siku ya Jumapili iliyopita katika klabu ya usiku ya Club Billicanas ambapo wakati anatumbuiza kukatokea tukio la kusikitisha lililopelekea mpenzi wake, ambaye anajulikana kama Mama Steve kuswekwa lupango kwa kumpiga chupa msichana ambaye inasemekana alikuwa mpenzi wa zamani wa Barnaba aliyekuwa akionyesha ishara za wazi wazi za kimapenzi.

Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari vilivyokuwepo katika Club hiyo ya usiku, baada ya kuona hivyo, Mama Steve alichukua chupa na kumpiga nayo msichana huyo ambaye alipasuka vibaya usoni na kuwahishwa polisi na kisha hospitali ili kupata matibabu, na kisha Mama steve ambaye ndiye mpenzi wa Barnaba kupelekwa katika kituo cha polisi Oysterbay ambapo inasemekana kuna maridhiano kati ya pande zote tatu na kila kitu kinakwenda sawa.

Baada ya tukio hilo, inadaiwa kuwa kuna msichana mwingine anayeishi maeneo ya Mwananyamala wilaya ya Kinondoni ambaye anamtafuta Barnaba ili ambwagie mtoto kwakuwa anadai amekuwa hampi sapoti yoyote katika matunzo.

Binti huyo, inavyosemekana anatafuta nafasi ambapo msanii huyo atakuwa na shoo na yeye atatafuta upenyo wa kwenda kumbwagia mtoto huyo!!

Tunachojaribu kujiuliza hatujui ni mdudu gani aliyeingia katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya husasan Bongo Flava kwakuwa ‘trends’ za sasa zinaonyesha matukio yasiyo ya kawaida kwa wasanii wetu yameendelea kushika kasi na hili la Barnaba ni moja ya vitu vinavyotufanya tujiulize, je! kama itatokea hivyo mambo hayo hayawezi kupoteza focus ya msanii? Au wasanii wanaoonekana kukomaa na hivyo kuzima nyota zao za kisanii wakiwa bado hawajadumu vya kutosha?

No comments:

Post a Comment