Wednesday, December 5, 2012

"WASANII WA BONGO WANAISHI MAISHA YA STAREHE SANA" BELL 9

IDADI kubwa ya wasanii wa muziki na filamu nchini Tanzania, wamekuwa na tabia ya kutangaza kumiliki mali na kuishi maisha ya kifahari wakati ukweli wa maisha yao si huo. 

Staa wa muziki, Belle 9, anasema kuwa tatizo la wasanii wengi kufilisika kisanaa limetokana na kuishi maisha ya kufikirika huku wakiwa na mitazamo hasi kuwa msanii anapaswa kuishi maisha ya kifahari. 

"Wamejikuta wakiishi maisha yasiyo yao na hata kutangaza mali ambazo si rahisi kuzimiliki. Hii yote imetokana na wasanii kuishia kufanya kazi moja na kusahau uwekezaji," anasema. 

"Msanii anavyopata fedha nyingi hatua ya kwanza huwa ni kununua gari na kuishi maisha ya kifahari na wengi wetu tunajisahau kuwekeza katika biashara na mambo mengine yaliyo na maana. 

"Kimsingi msanii anapaswa kuwa na jambo jingine analolifanya zaidi na sanaa. Kama hauko hivyo hakika mwisho wa siku tegemea kufulia (kufilisika)." 

Belle 9 ambaye ni mfanyabishara mjini Morogoro anasema kukaa kwake kimya katika tasnia ya muziki kwa kipindi kifupi sasa, kumetokana na kujipanga kikamilifu ili kuhakikisha anafanya kazi zinazokubalika na wengi. 

"'Anaishi Naye' ndio wimbo wangu wa mwisho kuutoa nikiwa na Ben Pol, lakini hivi sasa nipo chimbo nikiandaa kazi mpya ambayo nitaiachia kabla ya Krismasi, licha ya hilo pia biashara kidogo ilinifanya niwe bize," alisema. 

Msanii huyo alitamba na wimbo wa 'Sumu ya Penzi' mwaka 2009, ameendelea kubaki kwenye chati mpaka sasa na anavuma na video yake ya "Anaishi Naye". 

Sumu ya Penzi ulitoka kabla ya Masogange, Wewe ni Wangu, Ananifaa, Nilipe Nisepe na Anaishi Naye ambazo ameziimba kwa umahiri wa hali ya juu. 

No comments:

Post a Comment