Monday, January 28, 2013

Dr Cheni: Niko tayari kumtolea Lulu dhamana ya shilingi milioni 20



Muigizaji wa Bongo Movie Dr. Cheni amesema yeye ni miongoni mwa watu walio tayari kumdhamini muigizaji mwenzie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye leo hii mahakama kuu ya Tanzania imempa nafasi ya dhamana.

Lulu ambaye kwa zaidi ya miezi saba yupo mahabusu katika gereza la Segerea anakabiliwa na kesi ya mauaji dhidi ya marehemu Steven Kanumba.

Akiongea na Clouds FM leo katika mahakama kuu ya Tanzania ambapo kesi hiyo inasikilizwa, Dr Cheni ambaye yupo karibu na familia ya Lulu katika kipindi chote cha kesi hiyo amesema masharti yote ya dhamana hiyo yanatekelezeka.

“Kwa mfano kama hiyo wamesema kwamba kuna dhamana ya milioni 20 na mtu mwingine milioni 20 mimi ninaweza nikajitoa katika mmoja wapo katika upande huo,” alisema Cheni.

“Masharti mengine sidhani kama ni magumu kwasababu kila kitu kiko okay sidhani kama kitashindikana sasa hatujajua msajili atakapopata anatoa leo ama atamtoa lini sababu na yeye lazima apate muda wa kupitia yawezekana ana mafaili mengi juu ya meza.”

Cheni amesema masharti hayo yaliyowekwa wanaweza kuyatimiza leo hii. Masharti mengine ya dhamana hiyo ni pamoja na Lulu kurudisha hati yake ya kusafiria, haruhusiwi kutoka nje ya Dar es Salaam na atatakuwa kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya mwezi.

No comments:

Post a Comment