Tuesday, January 29, 2013

Risasi 20 zamkosa Rick Ross! Nani anataka kumuua?



Rick Ross ana bahati kuwa hai.Teflon Don huyo jana amekikwepa kifo baada ya mtu asiyejulikana kuishambulia kwa risasi gari yake aina ya Rolls-Royce alipokuwa barabarani huko Fort Lauderdale, Miami asubuhi ya jana.

Polisi wa Ft. Lauderdale wamedai kuwa tukio hilo lilitokea mida ya saa 11 alfajiri ambapo Ross alikuwa amekaa nyuma ya Rolls Royce hiyo yenye rangi ya silver.Baada ya kusikia risasi hizo, mamlaka zinasema Ross na mtu waliyekuwa naye aitwaye Shateria L. Moragne walijaribu kukwepa lakini alijikuta akikosa control na kwenda kugonga jingo.
WSVN-TV -

Kwa mujibu wa gazeti la Miami Herald, Ross alikuwa ametoka kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutumiza miaka 37.
Hakuna aliyeumia kwenye tukio hilo.

Polisi bado hawajapata sababu za mtu huyo kutaka kumuua Rick Ross ambapo mashuhuda wanadai jumla ya risasi 20 zilipigwa na hakuna hata moja iliyoifikia gari hiyo.Hata hivyo Herald limedai kuwa risasi kadhaa zilipiga majengo ya karibu ikiwemo moja iliyopiga dirisha la mgahawa ambao Rick Ross alikuwa ametoka kula.

Mwishoni mwa mwaka jana Ross alisitisha tarehe ya ziara yake kufuatia vitisho vya kuuawa.

No comments:

Post a Comment