Kebby Omary ambae ni msemaji na ndugu wa Rankeem Ramadhani anasema ‘Jumapili saa tano nilipigiwa simu kwamba kadondoka maeneo ya Meeda Sinza na akapelekwa hospitali ya Palestina Sinza na kuruhusiwa baada ya matibabu, alikua analalamika tumbo linamuuma lakini aliruhusiwa baada ya kupangiwa sindano za masaa, akawa anaomba maji ya kunywa na maziwa kwa sana na baadae akapendekeza achomwe sindano za maumivu lakini daktari hakuruhusu’
‘Jumatatu usiku mke wake alinipigia simu kwamba hali ya Rankeem inazidi kuwa mbaya na anabadilika, tulipomleta hospitalini Palestina wakaamua kumpeleka Mwananyamala hospitali ambako madatari waliamua kumpiga x-ray ambapo ilionekana utumbo wake umetoboka hivyo apelekwe kwenye ngazi inayofata haraka, asubuhi ya leo November 6 2013 akafanyiwa opareshen lakini baada ya dakika kama 120 Madatari wakasema sukari yake na presha vimeshuka inabidi awekewe oxygen, zoezi ambalo halikufanikiwa hivyo Rankeem akafariki dunia’ – Kebby
Bado haijajulikana Dj huyu maarufu kupitia Media mbalimbali Tanzania atazikwa wapi na saa ngapi, mipango bado inaendelea kufanyika.
SAA- TIME
GENERATION FM ONLINE
Wednesday, November 6, 2013
Taarifa kuhusu kifo cha Dj Rankeem Ramadhan
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment