Wednesday, September 19, 2012

TID ALILIA FIESTA.....!!!

Khaleed Mohamed aka TID now ameamua kuwa kutoa ya Moyoni katika kila jambo linalomkera. Siku moja baada ya kukaririwa akizungumzia juu ya issue yake dhidi ya Ali Kiba, leo ‘MNYAMAAAAAA’amezungumzia juu ya suala lake la kutokuwepo katika list ya wasanii wanao-perform katika the biggest music concert in Tanzania Fiesta. Kupitia his official facebook account TID ameandika status inayosomeka kama ifuatavyo: “I wiSh I coUld maKe the Guy Who does the FieSta Listing be oN my SiDe some PeoplE are workin verY Hard to juSt makE me Look like Criminal so I can not be on List Lakini Mungu atanipa Better than Fiesta tho its Been 5 years am nt Part of It”. Kwa maana hiyo owner huyo wa Top Band analalamika kwamba ana kila sifa ya kuwa mmoja ya wasanii wanaopanda katika jukwaa la tamasha hilo linaloendelea hivi sasa, lakini kwa sababu tofauti watu wanaoshughulika na kupanga listi ya wasanii wamekuwa wakimpotezea Mnyama kwa takribani miaka mitano iliyopita pamoja na kuwa hit songs nyingi ndani ya kipindi hicho

I-View Studio kurekodi Video mpya ya Diamond Platnumz

KAMPUNI I-View Studios ya mjini Dar es Salaam imeshinda mchakato wa kurekodi video mpya ya msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambayo usaili wake utafanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge, Dar es Salaam.

Akizungumza mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema I-View imepata nafasi hiyo kutokana na kiwango kikubwa cha video kadhaa ilizofanya lakini pia vifaa ilivyo navyo na uwezo wa wafanyakazi wake.
“Siku zote kila mtu anaangalia kitu kizuri, Diamond ametaka kufanya mapinduzi katika tasnia ya muziki, lakini kufanya mapinduzi kunahusisha vitu vingi, tungo zake yeye kama msanii, studio anayorekodia watu watakaoshiriki kwenye video yake kampuni itakayorekodi video pia, lakini mwisho wa siku I-View chini ya Raqey Mohamed ndio imeshinda nafasi hiyo.

“Raqey anafahamika kwa kazi zake pamoja na kurekodi matangazo mbalimbali ya Televisheni, picha mnato lakini pia video za wasanii Taznim ya Kwasakwasa, Utanikumbuka ya Suma Lee ni baadhi ya kazi ambazo zinaonyesha uwezo alionao lakini pia Diamond na timu yake tumeweza kuona vifaa vipya na vya kisasa ambavyo Raqey anavyo kwa sasa na hakuna kwa Afrika Mashariki na Kati,” alisema.

Kwa upande wake Raqey ambaye ni Mkurugenzi wa I-View alisema anahitaji kuifanya kazi hiyo kuwa tofauti ili kusukuma mbele sekta ya mawasiliano na muziki kwa ujumla.
“Sisi kama I-View tunafurahi kufanya kazi na Diamond, ni msanii mzuri na mkubwa ambaye kazi zake zinaonekana, hatutamuangusha na mashabiki na wasanii wengine wasubirie kazi itakapotoka,” alisema.

I-View pia watashiriki katika mchakato wa kupata watu watakaonekana kwenye video hiyo ambayo ni kwa mara ya kwanza nchini kutafanywa usaili wa washiriki. Usaili huo utafanyika Jumamosi katika ukumbi wa Nyumbani Lounge ambao unamilikiwa na mwanamuziki Lady Jaydee. Majina ya majaji wataochuja yatanatarajiwa kutangazwa leo.

Friday, September 14, 2012

Diamond Platnumz kufanya usaili watakaonekana video yake mpya

MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul, anatarajia kufanya usaili kwa ajili ya watu watakaotumika katika kurekodi video ya wimbo wake mpya ambao utaachiwa hivi karibuni.

Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema mjini Dar es Salaam kuwa Diamond amefikia uamuzi huo katika kuhakikisha kazi zake zinafanyika katika kiwango cha kimataifa.

“Jumamosi ijayo tutafanya usaili wa watu ambao wataonekana kwenye video hiyo, hii ni mara ya kwanza kwa kitu kama hiki kufanyika nchini kwetu ingawa wenzetu Ulaya wamekuwa wanafanya hivyo na wanaonekana wanakuwa wanalipwa tofauti na video nyingi za wasanii wa hapa kwetu na hao watakaochaguliwa kwenye video hiyo watalipwa pia,” alisema.

Akizungumzia kuhusu video hiyo, Mwendapole alisema itarekodi ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha inakidhi matakwa ya soko ambalo msanii huyo analiangalia kwa sasa huku video hiyo ikifanya na kampuni bora kabisa Tanzania.

Kwa upande wake Diamond alisema lengo kubwa la kufanya hivyo ni kuleta mapinduzi katika sekta ya muziki nchini lakini pia kutengeneza ajira kwa ajili ya wasichana na wavulana ambao wako mitaani lakini wanapenda muziki.

Diamond ambaye alikuwa nchini Marekani wiki iliyopita anatarajiwa tena kwenda Marekani kwa ajili ya onyesho moja la muziki.

Msanii huyo alifanya mapinduzi katika medani ya muziki wa bongo baada ya kufanya onyesho lake alilolipa jina la Diamond’s are Forever pale Mlimani City ambapo katika shoo hiyo aliifanya mwenyewe na kiingilio kikiwa sh 50,000 jambo ambalo halijawahi kufanyika katika ulimwengu wa muziki nchini.

Diamond Platnumz kufanya usaili watakaonekana video yake mpya

MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul, anatarajia kufanya usaili kwa ajili ya watu watakaotumika katika kurekodi video ya wimbo wake mpya ambao utaachiwa hivi karibuni.

Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema mjini Dar es Salaam kuwa Diamond amefikia uamuzi huo katika kuhakikisha kazi zake zinafanyika katika kiwango cha kimataifa.

“Jumamosi ijayo tutafanya usaili wa watu ambao wataonekana kwenye video hiyo, hii ni mara ya kwanza kwa kitu kama hiki kufanyika nchini kwetu ingawa wenzetu Ulaya wamekuwa wanafanya hivyo na wanaonekana wanakuwa wanalipwa tofauti na video nyingi za wasanii wa hapa kwetu na hao watakaochaguliwa kwenye video hiyo watalipwa pia,” alisema.

Diamond Platnumz kufanya usaili watakaonekana video yake mpya

MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul, anatarajia kufanya usaili kwa ajili ya watu watakaotumika katika kurekodi video ya wimbo wake mpya ambao utaachiwa hivi karibuni.

Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema mjini Dar es Salaam kuwa Diamond amefikia uamuzi huo katika kuhakikisha kazi zake zinafanyika katika kiwango cha kimataifa.

“Jumamosi ijayo tutafanya usaili wa watu ambao wataonekana kwenye video hiyo, hii ni mara ya kwanza kwa kitu kama hiki kufanyika nchini kwetu ingawa wenzetu Ulaya wamekuwa wanafanya hivyo na wanaonekana wanakuwa wanalipwa tofauti na video nyingi za wasanii wa hapa kwetu na hao watakaochaguliwa kwenye video hiyo watalipwa pia,” alisema.

Wednesday, September 12, 2012

BABY MADAHA AONGEZA UKUBWA WA MATITI

KATIKA kusaka mvuto wa kimahaba, msanii wa filamu na muziki, Baby Madaha ameamua kuongeza ukubwa wa matiti yake (angalia picha).
Akipiga stori na Tollywood Newz, juzikati jijini Dar es Salaam, Baby alisema amefikia uamuzi huo kwa sababu wanaume huvutiwa zaidi na matiti na makalio makubwa.
“Najua Wabongo wanaweza kushangazwa na uamuzi wangu, lakini ni mambo ya kawaida kabisa kutafuta mvuto wa mahaba. Nimeanza na matiti, baadaye nitakwenda a makalio,” alisema.
Alipotakiwa kutaja hospitali aliyofanya upasuaji huo alijibu kwa kifipi: “Ni siri, siwezi kuitaja ila iko Nairobi (Kenya).”

WEMA ALIZWA TENA!

BEAUTIFUL Onyinye wa Bongo, Wema Isaac Sepetu, hivi karibuni alijikuta akipata wakati mgumu baada ya kukombwa vioo vya gari lake aina ya Toyota Mark X na vibaka wa Moshi, Kilimanjaro, Risasi Mchanganyiko lina habari kamili.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni ndani ya Viwanja vya Chuo cha Ushirika ambapo staa huyo alikuwa amehudhuria uzinduzi wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Akiwa katika burudani hizo, Wema ambaye muda mwingi alionekana kuwa mtu mwenye furaha ghafla alibadilika na kuishiwa na furaha alipolikuta gari lake likiwa limekongolewa vioo vyote vya pembeni.

Gazeti hili lilizungumza na Wema kuhusu tukio hilo ambaye alionekana kushangazwa na tukio hilo na kusema kuwa hakutarajia kukutana nalo kwa kuwa alikuwa akiwaheshimu sana watu wa Moshi.
“Imeniuma sana baada ya kukuta gari langu limekongolewa, wameiba vioo na ukiangalia nipo ugenini, halafu magari ni mengi yaliyokuwa yamepaki uwanjani, kwa nini yasiibiwe hayo mengine wakaiba langu tu, dah! imenikera sana,” alisema Wema kwa uchungu.
Hilo ni tukio lingine la Wema kulizwa, alishawahi kuibiwa nyumbani Sinza jijini Dar baada ya wezi kuruka ukuta na kumkomba baadhi ya vitu vya thamani, pia alishawahi kuibiwa vitu vingine ndani ya gari Uwanja wa Taifa.