Monday, October 8, 2012

Sumaye: Sina vita yoyote na Lowassa "Akanusha kufanya kuzungumza na CHADEMA" Adai kuanguka NEC ni tiketi ya mapambano zaidi


WAZIRI Mkuu mstaafu, Bw. Frederick Sumaye, amekanusha uvumi uliosambaa katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa ametangaza vita na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bw. Edward Lowassa kama atachukua fomu ya kuwania urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema taarifa hizo hazina ukweli wowote bali ni za kutungwa kwani hajawahi kuzungumza lolote juu ya Bw. Lowassa, wala kuzungumza na mtu yeyote kuhusu jambo hilo.

Bw. Sumaye aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika mkutano wake na waandishi wa habari ili kufafanua masuala mbalimbali likiwamo suala la rushwa katika uchaguzi wa kuwania Ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), Jimbo la Hanang', mkoani Manyara.

Alidai kushangazwa na jinsi habari hizo zilipotokea na akawataka waandishi wa habari kuwa makini na wasikubali kutumiwa na wanasiasa wanaosaka urais 2015.

“Kuna baadhi ya magazeti yaliandika Sumaye kulipua bomu, mengine Sumaye kupasua jipu na kibaya zaidi, hivi majuzi gazeti moja likaandika Sumaye atangaza vita na Lowassa, ninachosema mimi sina jipu wala bomu la kulipua.

“Mimi sina ugomvi na Lowassa, hata nikiamua urais 2015 sitafanya hivyo kwa ajili ya mtu bali kwa masilahi ya Taifa,” alisema.


Kuteta na CHADEMA

Bw. Sumaye pia alishangazwa na habari iliyoandindwa na gazeti moja (bila kukitaja jina), kikidai alitetea (kufanya mazungumzo), na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

“Sijawahi kuzungumza na CHADEMA kuhusu kuhamia chama chao, hata kama ningetunana nao, ufike wakati wapinzani wasionekane kama maadui.

“Habari hiyo ni ya kutengeneza pamoja na picha iliyowekwa mbele ya gazeti nikiwa na Mbowe ili nionekane nateta naye, namuomba Mwenyezi Mungu jambo hili lifahamike ni uvumi tu ili tusije tukaiingiza nchi katika matatizo,” alisema Bw. Sumaye.

Uchaguzi NEC Hanang'

Akizungumzia kuhusu uchaguzi huo, katika Jimbo la Hanang', Bw. Sumaye alisema alipoteza nafasi hiyo kwa sababu uchaguzi huo ulitawaliwa na vitendo vya rushwa hivyo kumuathiri kwa
kiasi kikubwa.

Alisema mbali wajumbe kupewa rushwa pia yalikuwepo makundi aliyoyahita ya 'kiharamia', ambayo yalikuwa yakiwahamisha wajumbe nyakati za usiku ili wasipige kura.

“Mambo yaliyotokea Hanang', yalijitokeza sehemu nyingi lakini tofauti ni kwa ukubwa gani na nani yalimkuta,” alisema.

Aliongeza kuwa, pamoja na kwamba vitendo vya rushwa vilikuwepo siku za nyuma, safari hii hali ilionekana kuwa mbaya zaidi kwa sababu ya mitandao iliyokuwa ikisambaza fedha katika maeneo mbalimbali ili kuwang'oa wanasiasa hasa wanaokemea maovu.

Alisema zamani watu walikuwa wakienda wenyewe na kutoa fedha kwa wakazi wa eneo husika ili wachaguliwe lakini sasa hali hiyo imebadilika ambapo baadhi ya watu aliodai kuwa wanasaka urais kinguvu, wamejenga mtandao wa kununua wapiga kura.

“Kwa sasa kuna mtandao wa kuonga wapiga kura tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo mtu alikuwa akienda eneo husika na kuwapa fedha wapiga kura ili wachaguliwe,” alisema Bw. Sumaye akinukuu baadhi ya hotuba alizowahi kuzitoa katika matukio mbalimbali akikemea vitendo vya rushwa.

Hata hivyo, alipobanwa na waandishi wa habari kama anaweza kuutaja mtandao huo na eneo ambalo wajumbe walipewa rushwa Bw. Sumaye alikataa kata kata kuzungumzia zaidi suala hilo.

“Pamoja na kufanyiwa vitendo hivi, sitafikisha malalamiko yangu katika vikao vya chama wala kukata rufaa kwani yaliyojitokeza yalikuwa yakifahamika pia itaonekana nipo ndani ya CCM
kwa ajili ya vyeo.

“Mimi ni mwana CCM, nina imani na chama changu ambacho kiliunganishwa na vyama vya TANU na ASP, sipo ndani ya chama kwa ajili ya kutaka vyeo,” alisema Bw. Sumaye na kuongeza;

“Rushwa haizalishwi na demokrasia bali tunaizalisha wenyewe kwa sababau zetu za kijinga, nchini Marekani na Uingereza kuna demokrasia, mbona hatusikii vitendo hivi,” alihoji Bw. Sumaye.

Alisema kama wapiga kura wasipokuwa makini, Taifa litaambulia viongozi waliochaguliwa kwa nguvu za fedha badala ya utashi wa wananchi wenye haki ya kuchagua kiongozi wanayempenda.

Bw. Sumaye alisema katika nchi zenye demokrasia, wapiga kura huchagua kiongozi wanayempenda na mwenye uwezo lakini katika nchi zilizopondeka kwa rushwa, fedha ndio inayochagua viongozi
na kazi ya wapiga kura ni kupiga mihuri tu.

Alihadharisha hali hiyo na kudai kuwa, nchi nyingi zimeingia katika machafuko kutokana na chaguzi za aina hiyo na kushauri wale wanaopiga kelele kukemea vitendo hivyo vya rushwa waungwe mkono badala ya kusakama.

Aliwashauri viongozi ndani ya CCM, wajirekebishe kabla wananchi hawajachoshwa na hali hiyo na kuamua kuingia mitaani.

“Wananchi watachoshwa na hali hii, hawawezi kuvumilia mambo haya kama yataendelea ipo siku watasema inatosha, wakifikia hatua hiyo hali itakuwa mbaya zaidi,” alisema.

Kuteteleka kisiasa na hatma ya kuwania urais 2015

Bw. Sumaye aliulizwa kuanguka kwake NEC, pengine pamemfanya ateteleke kisiasa na kuathirika katika mbio za kuwania urais 2015, ambapo akijibu swali hilo alisema, hali hiyo imemuongezea nguvu na akaahidi kuendeleza mapambano akiwa ndani ya CCM.

“Kuangushwa kwangu ujumbe wa NEC kumenipa nguvu zaidi, wala sijateteleka kisiasa bali nitaendelea kupambana na maovu nikiwa ndani ya chamachangu CCM,” alisema Bw. Sumaye.

Alisema hata akiamua kuwania urais 2015, ingawa bado hajatangaza dhamira hiyo, matokeo hayo yamemrahisishia njia kwani kama angepata ujumbe wa NEC, ingemuwia vigumu kujitosa katika
mbio hizo.


Friday, September 28, 2012

KICHUPA CHAPEWA HIKI HAPA MZIGO UNAITWA BANDIA -- NI MCHIZI KUTOKA KENYA

Msanii - PEWA ABAGENGE
Song - BANDIA
Label - AUDIO KUSINI

Bandia ni neno la kiswahili likiwa na maana ya FEKI mchizi kalitumia kwa kufikisha ujumbe kwa watu bandia waliotuzunguka katika jamii kwa mfano marafiki, wachungaji na hata wanasiasa. Ebana eeh...!! Bonge la mzigo liskilizeni
HISTORIA KUHUSIANA NA MCHIZI
 
PEWA ABAGENGE
NAMES: Emmanuel Wanjala 
AGE: 22
STAGE NAME: PEWA ABAGENGE
MUSIC GENRE: NewSkool Genge
RECORDING LABEL: Audio Kusini
BASE: Nairobi

BACKGROUND INFO;

Pewa was born 22 years ago and was raised in Western Kenya at Webuye. He attended St.Mary’s Kibabii in Bungoma.

MUSIC JOURNEY;
He started rapping back then while in high school. During those days, Pewa used to remix the already established artistes songs and then perform during schools functions. After high school, he joined Audio Kusini Studios which is located at Kahawa Wendani along Thika Road. It’s under the management of Audio Kusini that Pewa has managed to release four tracks; Mwisho WA Mwezi, Kijiji Na Jiji, Nipeni Kura Zenu and recently Cheza Kinanda. He is also set to release more singles and collaborations soon.
ROLE MODELS AND INSPIRATION
Musically, I look up to artistes like Nonini, Prof. Jay and Fid Q (Tanzania) and internationally the likes of Eminem Akcent and Edwards Maya. M y music inspiration is drawn from daily happenings and trends.
DISCOGRAPHY;
1.       KIJIJI NA JIJI feat Blaq Childs
2.       NIPENI KURA ZENU
3.       HIPHOP GENGE  feat by Kaktus
4.       CHEZA KINANDA feat Erica
ASPIRATION
To become among the Africans most influential artistes.

Sikiliza wimbo huu wa CHALII MTOTO WA BIBI aliyemwimba DOGO JANJA kuwa ni DOGO MBUMBUMBU

ZITTO KABWE: 2015 SITAGOMBEA UBUNGE


Baada ya kusikia kupitia vyombo mbali mbali vya habari kuwa Mh mbunge wa Kigoma Mjini Zitto ametangaza kuwania kiti cha uraisi ifikapo mwaka 2015, Zitto ameendelea kusisitiza msimamo wake kupitia mtandao wa jamii wa Facebook
Zitto Kabwe
Narudia, mwaka 2015 sitagombea Ubunge. Nitafanya kampeni ya Urais, ama mimi kama mgombea wa chama changu CHADEMA au kama mpiga debe wa mgombea wa chama changu. Miaka 10 ya Ubunge inatosha na kwa ngazi hiyo ni vema niwaachie wengine wasukume mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbo na mkoa wetu. Huu ndio uamuzi wangu wa mwisho na nimeshawaeleza wananchi wa Jimbo langu na mkoa wa Kigoma toka mwaka 2005

Thursday, September 20, 2012

Nay wa Mitego azungumza na Hot Mix ya EATV


Diamond Platnumz: Nataka kutengenza ajira kwa vijana wenzangu

MSANII wa Kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema amedhamiria kutoa ajira kwa vijana wengi wa kitanzania kupitia muziki huku pia akileta mapinduzi katika sekta hiyo nchini.
Diamond ambaye ni msanii ghali zaidi kwa sasa Tanzania, amesema kuna watu wengi wenye vipaji ambao wako mtaani au wako katika sekta nyingine lakini hawajui wafanyeje ili kufikia ndoto zao jambo ambalo linahitaji watu wengine wawasaidie kuwafikisha pale wanapotaka.
“Kuna tatizo ambalo lipo katika mambo ya mitindo, muziki. Watu wengi wanachukulia kama uhuni, wengi wanaona kama kuuza sura, yaani mtu aonekane kwenye video ili apate umaarufu, tunatakiwa kubadilisha mawazo haya, Ulaya hata hapo Afrika Kusini wanaonekana kwenye video wanalipwa.

“Mimi nitawalipa wote watakaonekana kwenye video yangu, tutakapofanya usaili kesho wale watakaochanguliwa watalipwa, lakini pia hii inaweza kuwa ni kufunguliwa milango kwenye sekta nyingine, wapo wanaoweza kuonekana wanafaa kwenye matangazo ya biashara, hawa watapata kampuni ambazo zinaweza kuwatumia.
“Katika majaji watakuwepo Raqey Mohammed wa I-View Studios, hawa wanafanya kazi nyingi za matangazo, movie, atakuwepo pia Ally Rehmtulah huyu ni mbunifu anaweza kumuona mtu na akasema huyu anafaa kwa sekta yake, Sammy Cool ni densa na mwalimu hata Missie Popular yeye ni mwandishi na mwanamitindo wanajua wapi kwa kuwafikisha watu wengine’ alisema.
Msanii huyo alisema mafanikio aliyo nayo ya kumiliki nyumba, magari na kujulikana kwake yametokana na muziki, hivyo ana uhakika wapo watu wengine pia kupitia yeye na wanamuziki wengine kama yeye wanaweza kufaidika na kufikia mafanikio kama aliyoyapata.

Diamond alisema usaili huo unafanyika kesho  pale nyumbani Lounge kuanzia saa tano asubuhi. Hii ni mara ya kwanza kwa msanii wa nchini kufanya usaili kwa ajili ya watu watakaonekana kwenye video yake.
Diamond pia ndiye msanii wa kwanza wa muziki wa kizazi kipya kuandaa shoo yake mwenyewe na watu kulipa kiingilio cha sh 50,000. Diamond alifanya hivyo kwenye onyesho alilolipa jina la Diamond are Forever pale Mlimani City, Dar es Salaam.


Majaji usaili wa video ya Diamond watangazwa



MSANII wa Kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ataongoza jopo la majaji wengine wanne kwa ajili ya kupata wasichana na wavulana watakaoshiriki kwenye video yake mpya.

Usaili wa watu hao utafanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge, mjini Dar es Salaam ambao wote watakaochaguliwa kuonekana kwenye video hiyo itakayorekodiwa na kampuni ya I-View Studios watalipwa.

Katika orodha hiyo, yupo mbunifu wa mitindo wa kimataifa, Ally Rehmtullah ambaye hivi karibuni alizundua mavazi yake mapya katika hoteli ya Serena, yupo pia Raqey Mohamed ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya I-View Studios,pia Creative Director, Sammy Cool ambaye ni mwalimu wa dansi na blogger maarufu Missie Popular.

Akizungumza mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema majaji hao wamechaguliwa kutokana na kuhusika kwao na shughuli za sanaa kila siku.

“Diamond ndiye mwenye video na ni mwanamuziki, Raqey ndiye atakayerekodi video, lazima ajue watu ambao ana wataka kwenye hiyo video, ameshafanya kazi kama hizi mara nyingi, ni mpiga picha wa kimataifa, Sammy Cool ni densa maarufu na mwalimu ambaye amewafundisha watu wengi katika ulimwengu wa kucheza nchini, wengi watakuwa wakimfahamu tangu enzi za Bombeso, THT na mashindano mbalimbali ya urembo, amekuwa pia akitoa ushauri nasaha.

“Kwa upande wa Ally ni mbunifu wa mitindo wa kimataifa, ameshafanya kazi mpaka ulaya, ana uzoefu mkubwa kutokana na kazi zake kwa hiyo kuwepo kwake kutasaidia pia vipaji vingine kuonekana, Missie Popular yeye ni mwandishi, mwanamitindo kwa hiyo kama mtu wa habari ana mchango wake katika kuibua vipaji pia,” amesema.

Mwendapole amesema usaili huo utaanza saa tano kamili asubuhi na kwamba baada ya usahili huo wale watakaochaguliwa watafahamishwa mazoezi yatakuwa wapi na baada ya hapo kazi ya kurekodi video hiyo kuanza.

Video hiyo ambayo wote watakaochaguliwa kuonekana watalipwa, itarekodiwa maeneo mbalimbali nchini pamoja na sehemu nyingine nje ya bara la Afrika ili kuipa ladha tofauti. Kampuni ya I-View ndio imeshinda mchakato wa kurekodi video hiyo.

Tayari kampuni hiyo imeweza kutengeneza video kadhaa za kiwango cha kimataifa ikiwemo Kwasakwasa Tazneem, Utanikumbuka ya Suma Lee pamoja na matangazo mbalimbali ya biashara. I-View pia ndiyo inatengeneza kava za wasanii mbalimbali Bongo Movie ambao wanafanya kazi na Steps Entertainment.