Baada ya ngoma ya Diamond kuachiwa jana muda mfupi tu baadae nyimbo hiyo imeleta utata mkubwa kutoka kwa wasanii wawili tofauti ikishutumiwa kuwa ni idea ya wimbo wa Pasha aliomshirikisha Tunda Man upande wa beats na jina la wimbo ni H Baba kwa upande mwingine.
Wakizungumza na kituo cha Clouds Fm kupitia segment ya 255 ya kipindi cha XXl Pasha anasema alipigiwa simu na mshikaji wake akiambiwa kuhusu kufanana kwa nyimbo hizo na kwamba yeye pasha anasema alirekodi mwanzoni mwa mwaka huu na kwamba beat iliyotumika inafanana kwa asilimia 100 na nyimbo yake, wakati H Baba yeye anasema jina la wimbo huo ni kama jina la wimbo wake.
Akiongea na bongo5 mchana wa leo H Baba alikwenda mbali na kusema yeye alikuwa studio na KGT akirekodi wimbo wake aliomshirikisha Q Chief ndipo Diamond naye alifika hapo studio akiwa anaenda kufanya chorus ya nyimbo ya Shetta inayoitwa Nidanganye.
Anasema baada ya kuingia studio na kuwakuta wao yaani H Baba na Q chief Diamond aliusikia wimbo huo na kumwambia kuwa ameufagilia na kuwapa big up kwa kazi nzuri lakini anasema cha ajabu ameshangaa jana anaambiwa kuna wimbo unaitwa Nataka Kulewa na alipokwenda kucheki kwenye net akakuta ni kweli Diamond ameachia wimbo wenje jina hilo.
Akiongea kwa uchungu kupitia simu H baba amesema ameibiwa wimbo wake na Diamond ingawaje kwa kusikiliza wimbo wa Pasha upande wa beat na melodi hali inaonekana ni tet.
Swali la kujiuliza nani kati ya hao wawili Pasha na H Baba nani ameibiwa zaidi?
NATAKA KULEWA ---DIAMOND
AMEKUA ---PASHA FIT TUNDA MAN
No comments:
Post a Comment