Wednesday, November 14, 2012

Bhoke (BBA) ateuliwa kuwa balozi wa taasisi inayopambana na funza wa miguu (jiggers)


Aliyewahi kuwa mwakilishi wa Tanzania katika shindano la Big Brother Africa, 2011, Bhoke Egina ameteuliwa kuwa balozi mpya wa Tanzania wa taasisi ya Ahadi Trust Tanzania.


Bhoke alikuwa akisherehea siku yake ya kuzaliwa weekend iliyopita na kuitumia pamoja na rafiki zake kutumia siku hiyo kampeni dhidi ya funza wa miguuni.
Mguu ulioathiriwa na funza


Tukio hilo lilifanyika mjini Moshi ambapo mwenyekiti mtendaji wa Ahadi Kenya , Stanley Kamau alimtangaza Bhoke kama balozi wa Tanzania na kuonesha kufurahishwa kwake na mastaa wanaoguswa na kuhudumia jamii hasa katika mapambano dhidi ya funza ambao ni tatizo barani Afrika.
Mshindi wa BBA 2007, Richard, Bhoke Egina na Cecilia Mwangi wa Ahadi Kenya wakimhudumia mtoto aliyeathirika na funza

Hafla hiyo ilihudhuria pia na mshindi wa BBA mwaka 2007, Richard Bezuidenhout.Bhoke alikuwa ni miongoni wa washiriki wa mwaka 2011 wa BBA walioenda Thika nchini Kenya kuwasaidia watoto walioathiriwa na funza ambapo anasema hakulijua tatizo hilo mpaka alipowaona watoto hao.



No comments:

Post a Comment