Mamia ya watu leo wamejitokeza katika mazishi ya muimbaji mahiri wa Taarab nchini Mariam Khamis maarufu kama Paka Mapepe aliyefariki juzi wakati akijifungua. Mariam alifariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo mtoto wake alisalimika.
Marehemu Mariam Khamis
Mazishi hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu wa aina mbalimbali wakiwemo wasanii wengine wa muziki wa Taarab.
Miongoni mwa wasanii waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Khadija Kopa, Isha Mashauzi, Mzee Yusuph na mke wake Bi Leila,Nyota Waziri, Bi Hindu na wasanii wenzake wa kundi la TOT.
Mariam alikuwa muimbaji wa kundi la taarab la TOT na enzi za uhai wake aliwahi kuimbia katika makundi mbalimbali ya taarab ambayo ni pamoja na East Africa Melody, Zanzibar Stars na 5 Stars.
Marehemu Mariam Khamis ameimba nyimbo nyingi zinazofanya vizuri katika muziki wa Taarab zikiwemo ‘Huliwezi bifu’, ‘Raha ya Mapenzi’ na ‘Ndo basi tena’.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pepa peponi.
No comments:
Post a Comment