Friday, November 16, 2012

Wyre amuimbisha Kiswahili Alaine Laughton


Ukiambiwa kumtaja msichana anayefanya vizuri kwenye muziki wa reggae nchini Jamaica na duniani kwa jumla huwezi kumkwepa Alaine Laughton. Ni msichana mrembo ambaye weledi wake upo katika masuala ya benki lakini amebarikiwa sauti tamu inayoweza kumtoa nyoka pangoni.

Uimbaji wake wa reggae uliochanganyika na flava fulani tamu za R&B umemfanya asilinganishwe na msichana yeyote wa miaka ya hivi karibuni katika muziki huo. Good news kwa lugha yetu tamu ya Kiswahili ni kwamba mrembo huyo hivi karibuni atasikika akikiimba kwenye wimbo alioshirikishwa na mwanamuziki wa Kenya, Wyre.

Ngoma hiyo inaitwa Nakupenda pia ambayo juzi Wyre aliionjesha kidogo kwenye kituo cha radio cha Homeboyz na Alaine kusikika akiimba sehemu yake ya Kiswahili kwa ufasaha kabisa.

Tunaisubiri kwa hamu.

No comments:

Post a Comment