Pamoja na kuwa na single mbili tu hewani, Nai Nai na Baadaye, Ommy Dimpoz anafahamika na wapenzi wengi wa muziki nchini na jirani ya Tanzania utadhani ana miaka zaidi ya kumi kwenye muziki. Na sasa wakati wengi wakiusubiria ujio wake wa tatu, leo msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Omary Faraji Nyembo ametangaza kuwa ataachia single yake ya mpya wiki ijayo.
Akiongea na Bongo5 Ommy amesema single hiyo imetengenezwa katika studio za THT ambapo producer ni Imma the Boy. Kuhusu jina la wimbo amesema anataka kufanya surprise lakini amesema wimbo huo unazungumzia malavidavi kama kawaida.

No comments:
Post a Comment