Saturday, November 3, 2012

Sheria inaizungumziaje issue ya H.Baba na Diamond?


Awali ya yote tungependa kusema kuwa Bongo5 haijajuchukua upande wowote kati ya pande mbili zilizoingia kwenye mgogoro mkubwa wa wimbo ‘Nataka Kulewa’. Upande mmoja ukiwa wa Diamond na upande mwingine ukiwa wa Pasha na H.Baba. Dai la Pasha dhidi ya Diamond ni kufanana kwa beat ya wimbo wake na wimbo wa Diamond ambapo hapa mwenye kutakiwa kujibu zaidi ni producer wa wimbo huo ambaye ni Manecky.

Dai la H.Baba ni kuwa Diamond amemuibia wazo lake na jina la wimbo alioufanya mwaka jana. Kwa haraka haraka aliyeumizwa zaidi hapa ni H.Baba ambaye wimbo wake aliourekodi wenye jina hilo umeuliwa tayari na wimbo wa Diamond. Kama akiamua kuutoa hatakuwa na jipya kitu ambacho amesema hawezi kufanya. Jana (Nov 2) alikuja kwenye ofisi za Bongo5 akiwa na ushahidi wa wimbo huo kwakuwa wengi wamekuwa wakimshutumu kutafuta umaarufu kupitia issue hii bila kukumbuka kuwa alichofanyiwa ni kama mtu aje achukue wazo na jina la biashara/mradi wako na kuufanya wake. Haya ndiyo aliyoyaongea:


Baada ya kumsikiliza hapo juu, tukumbushie jambo tuliloanza nalo mwanzo kuwa kama chombo cha habari huru na kisicho na upendeleo hatujaegemea kwenye upande wowote katika vita hii ambayo haiwezi kuisha leo na tunajaribu kuzipa nafasi pande zote mbili kuzungumza. Kuhahakikisha hilo linafanyika, jana tumezungumza na uongozi wa Diamond kupitia meneja wake Raqey Mohamed wa I-View Media kutaka kupata machache kutoka kwao.

Ingawa mwanzo alisita kwa kudai kuwa mwisho wa siku hawapendi kupigizana kelele, aliahidi kutafuta nafasi ili Diamond aweze kuzungumza yake. Wakati tukisubiri hilo kufanyika, tungependa kutoa ufafanuzi mfupi wa jinsi sheria ya haki miliki inavyofanya kazi kwenye kesi kama hii hasa kwa upande wa lalamiko la H.Baba ambaye amesema atalipeleka suala hili kwenye mamlaka husika. Bahati mbaya kwake ni kuwa sheria hizi zinaweza kumnyima haki kwakuwa hazilindi wazo lililoibiwa na hakuna aliyelisikia kabla ya kazi ya pili (ya Diamond) kutoka.

Kwa mujibu wa FRANK.T.MUNAKU (blogger, Lawyer with Bachelor of law degree (Hons) from UDSM and PGD[Postgraduate Diploma in practical legal Training] from Law school of Tanzania, qualified to be an Advocate of the High Court and Subordinate Courts thereto but Currently working with the Tanzania judiciary serving as a Judge’s legal Assistant at the High Court Of Tanzania) amekielezea kipengele hicho kama ifuatavyo:

Kwa mujibu wa kifungu cha 3(3) cha Sheria hii wasanii wanaomiliki kazi za kisanii na wana hakishiriki pia watapewa ulinzi na sheria hii.Katika kifungu cha 4, msanii ametafsiriwa kama mwigizaji, mwimbaji, mwanamuziki, mchezaji (dancer) au mtu anayeigiza, kuchonga au kufanya maonesho jukwaani.

Hata hivyo, sheria hii kama sheria nyingine nyingi za hakimiliki, imetoa sharti kwa kazi za kisanii kulindwa na sheria hii na kigezo hiki ni kwamba kazi hiyo iwe katika hali ya kushikika, na kwa maana nyingine ni kwamba wazo/mawazo hayatalindwa na sheria hii hata kidogo.

Kwa mfano, kama A na B walio katika sehemu tofauti lakini wana wazo linalofanana la kutengeneza wimbo unaohusu foleni za magari, na A akawa wa kwanza kuingiza wimbo huo katika hali ya kushikika (katika minajili hii akawa ameurekodi studio), basi B hawezi kuja kumshitaki A kwa kuiba wimbo wake kwani yeye alikuwa na wazo tu na wakati mwenzake aliliweka katika hali ya kushikika.

Suala linakuja kuleta utata tena kwamba tayari wazo la H.Baba (kwa mujibu wake mwenyewe) kuwa wimbo huo alikuwa ameshaurekodi lakini ukabaki katika mfumo wa demo (wimbo ambao haujakamilika) kwa muda mrefu bila kutoka. Baada ya Diamond kutoa wimbo wake ndipo amejitokeza akiwa na ushahidi huo kuwa wazo lake limeibiwa. Kisheria anaweza kujikuta akitiliwa mashaka tena kwamba huenda demo hiyo ameirekodi haraka haraka baada ya Diamond kutoa wake, you never know!!!

Tunasuburi kuona issue hii itafikia wapi. Lakini ikumbukwe kuwa mambo kama haya katika nchi za wenzetu hugeuka kesi kubwa ambazo mlalamikaji huweza kupewa mamilioni

No comments:

Post a Comment