Diamond Platnumz ataendelea kuwa newsmaker kuliko msanii yeyote Tanzania. Hauwezi kupita mwezi bila kuibuka kitu kitakachomfanya aandikwe tena na tena. Katika picha iliyowekwa kwenye ukurasa wa Facebook wa msichana aitwaye Skyner Ally kuna picha inayomuonesha Diamond akiwa amelala usingizi wa pono na msichana anayedaiwa kuwa ni mtangazaji wa DTV, Penny Mungilwa aka Vj Penny. Picha hii inajieleza yenyewe kwa pozi walilolaa kuwa ni wapenzi ama ni one night stand? Wonders will never cease!! Ingia ndani kuona picha hiyo.
Hata hivyo tulipowasiliana na Penny alisema hiyo ni picha iliyopigwa walipokuwa kwenye scene ya movie wanayoigiza pamoja ambayo amesema hana uhakika lini itatoka! Penny na Diamond in a movie? If it’s true then tunaingojea kwa hamu!!
No comments:
Post a Comment