Thursday, January 24, 2013

Hemedy: Movie zangu zinaangaliwa sana tangu mfumo wa digitali uanze!!!


Mfumo wa digitali nchini umekuja na faida na hasara zake. Japokuwa hasara ni nyingi, kubwa ni kuwafanya wananchi wengi wenye kipato cha chini kukosa matangazo ya TV kwa kushindwa kununua ving’amuzi, wapo watu wanaonufaika na hali hiyo.

Tangu mfumo huo uanze inasemekana kuwa soko la filamu za Tanzania limeongezeka kwakuwa wananchi wasio na ving’amuzi wamekuwa wakinunua movie za kibongo kwa wingi ili kupoteza muda wawapo nyumbani. Ushahidi wa jambo hilo umetolewa na Hemedy ambaye anasema mfumo wa digitali umeongeza idadi ya warembo wanaompigia simu kusifia movie zake ukilinganisha na zamani.

“Tangia system ya Digital imeanza napokea simu nyingi sana za masista duu wanasifia movie zangu…kitambo walikua wanasema sijui movie zenu,” ametweet Hemedy.

Akijibu swali letu kama anamaanisha kweli, Hemedy amejibu, “true dat….it’s a good thing pia…wanathamini vya home.”

No comments:

Post a Comment