Mchekeshaji na muigizaji wa Tanzania Tumaini Martin ‘Matumaini’ yupo nchini Msumbiji ambako anasumbuliwa na tatizo la kuvimba tumbona miguu na mwili kukosa nguvu. Kutokana na hali hiyo muigizaji huyo anahitaji msaada wa nauli ili aweze kurudi na kuja kupata matibabu nchini.
THE BIG DAD imepata taarifa rasmi kutoka kwa mwenyekiti wa chama cha waigizaji taifa Michael Sangu aliyesema, “Msanii mwenzetu Matumaini anaumwa sana na bado mpaka sasa yupo Msumbiji na kitu ambacho kinamsumbua zaidi ni kuvimba tumbo na miguu na akiwa hana uwezo wa kujitibia wala nauli ya kuweza kurudi nchini”.
Taarifa za awali zinasema kuwa Matumaini aliingia nchini Msumbiji katika ziara ya kisanii akiwa huko alimpata jamaa akaamua kufanya maisha yake huko. Wenzake aliosafiri nao kwenda nchini humo Tanzania na yeye kuanza maisha mapya.
Kwa wale wanaopenda kumsaidia wanaweza kuwasilisha michango yao kutuma kupitia tigo pesa kwa namba 0718 951 355 kwa mwenyekiti Mike Sangu.
YOTE KWA HISANI YA BONGO5
No comments:
Post a Comment