Muimbaji mkongwe wa Kilimanjaro Band aka Wana Njenje Waziri Ally amesema muziki wa Tanzania umekua sana kibiashara lakini unaendelea kufa kitaaluma.
Akiongea na Bongo5, Mzee Waziri ambaye ni kiongozi wa bendi hiyo kongwe nchini Tanzania amesema kwa sasa muziki unafanyiwa promotion sana na hivyo kuufanya uuzike. “People are making money sasa hivi sio kama sisi tulivyoanza muziki wakati huo,” alisema. “Na ndio maana sasa unaona mfumko wa wanamuziki wapya ni wengi sana kila mmoja anajua akitoa wimbo mpya atapata hela yake atanunua gari, atanununua nyumba nk. Kwahiyo kibiashara unakua lakini sio kitaaluma, taaluma ya muziki inakufa. Kwasababu kila miaka inavyozidi kwenye wanamuziki wanapungua, nikisema wanamuziki naamanisha wale wanaojua taaluma ya muziki, either amekwenda shule kusoma muziki au anapiga tu muziki bila kusoma ama kwa kipaji lakini anapiga muziki kiusahihi.”:
Waziri amesema wanamuziki wa sasa wanapenda njia za mkato kutoka hali inayochangia kwa kiasi kikubwa taaluma ya muziki kushuka ama kufa na kuongeza kuwa Tanzania kwa sasa imeachwa nyuma na nchi zingine za Afrika Mashariki hususan Uganda.
“Music imehamia Uganda, ukisikiliza production za Uganda utasikia kuna watu wametuliza akili zao wamefanya arrangement na kuna music ndani yake, ukisikia uimbaji wa Uganda wanaimba, unajua kabisa hapa kuna waimbaji.”
No comments:
Post a Comment