Friday, February 1, 2013

Sumalee afiwa na baba yake mzazi, ashindwa kuhudhuria mazishi



Hitmaker wa Hakunaga, Sumalee, amefiwa na baba yake mzazi, Mzee Sadick Iddi. Taarifa hizo zimetolewa na yeye mwenyewe kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Hata hivyo Sumalee ambaye yupo nchini Uingereza hatoweza kuhudhuria mazishi ya baba yake yanayofanyika leo mchana. Mwaka jana msanii huyo alifiwa pia na mama yake mzazi.Tunampa pole kwa msiba huo.

No comments:

Post a Comment