Thursday, October 11, 2012

DIAMOND PLATNUMZ APIGA KAMPENI NGORONGORO CRATER

Diamond Platnam'z

SANII wa muziki wa kizazi kipya,Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewataka watanzania kulipigia kura bonde la Ngorongoro kuwa moja ya maajabu saba ya Afrika na pia kujenga tabia ya kutembelea vivutio vya utalii vya ndani.
Akizungumza mjini Ngorongoro, Diamond ambaye alikuwa huko kujionea bonde hilo ambalo ni la kipekee ulimwenguni, amesema hakuwahi kufikiria kwamba kuna sehemu nzuri ambayo hata watanzania wanaweza kwenda kutembea na kujionea vivutio vilivyopo.
“Hii ni mara yangu ya kwanza kufika hapa, lakini kwa kweli nimeshangazwa na jinsi palivyo pazuri, wanyama, mito ambayo inapita huku chini, mi huwa naona kwenye televisheni tu katika kile kipindi cha National Geography cha DSTV lakini sikujua kama mambo haya yapo kweli kwetu.
“Nawaomba watanzania wenzangu waweze kutembelea Ngorongoro na vivutio vyetu vya utalii kwa sababu kuna mengi ya kujifunza, leo kama isingekuwa Afrika sidhani kama kungekuwa na kipindi kama National Geography, na gharama za kuja huku si kubwa, hatupaswi kuogopa, hivi ni vitu ambavyo vinawezekana kabisa suala ni kujipanga,” amesema.
Amesema wenzetu kutoka Ulaya wamekuwa wakijipanga kuweza kutembelea sehemu Fulani jam bo ambalo linawafanya waweze kutembelea nchi nyingi kufanya utalii.
“Pamoja na kuja kupunguza mawazo lakini sehemu kama hii inasaidia kuelemisha, mwito wangu kwa watanzania wenzangu, mashule hata vyuo waweze kuja hapa, inakuwa rahisi zaidi kumfundisha mtoto kuhusu Simba, Twiga, au bonde la Ngorongoro kwa kumuonyesha hiki kiko hivi, nadhani kama watoto watakuwa wanasoma kwa vitendo hawawezi kushindwa mitihani yao kwa sababu kumbukumbu inabaki kichwani kwa kile walichokiona,” amesema.
Msanii huyo alikwenda Ngorongoro baada ya kumalizika kwa tamasha la Fiesta ambapo alikuwa mmoja wasanii waliofanya vizuri. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ilimualika Diamond huko. Ngorongoro ni moja kati ya vivutio vya Tanzania vinavyotakiwa kupigiwa kuingia katika maajabu saba ya Afrika
Diamond plutnim'z

OFFICIAL RELEASE: C-SIR MADINI "PAIN KILLER" (Audio & Lyrics))

Hello mambo vipi




Please pokea wimbo mpya wa Msanii C-SIR MADINI (Sisa) ambayo leo ndio tunai release rasmi kuanza kuchezwa katika radio stations. Video tayari ilitoka siku mbili zilizopita.

The story behind the existence of this song, ni kwamba kwanza ni wimbo ambao umeandikwa na kurekodiwa siku moja ilikuwa mwezi may 2012, baada ya hapo kazi ya umaliziaji wa beat pamoja na mixing ikaendelea kwa takriban wiki 2.

Idea ya wimbo huu, title na lyrics zote zimeandikwa na kidbwoy, na zina base katika chembechembe za true story zinazomhusu muandishi wa wimbo huu.

Maana ya wimbo huu ni kwamba, C-sir amepata kitulizo cha moyo wake ulioumizwa na mpenzi alietangulia, hivyo baada ya kumpata mtu alieamini kuwa ndio tulizo la moyo wake, huyo ndio akawa Pain Killer yake, lakini ni tofauti na pain killer zote unazozifahamu ambazo mara nyingi huwa zina uchungu wakati wa kumeza. Tofauti ya Pain Killer ya C-sir na Pain Killer za maumivu ya kichwa ni kuwa hii ni "PAIN KILLER/TAMTAM", licha ya kumtibu lakini bado ni tamu.

Hii ni ngoma ya 3 kwa C-sir Madini kuachia, baada ya KIFUNGO HURU iliyotoka kama single ya kwanza mwaka jana, iliyofuatiwa na NISHIKE MKONO aliyoitoa mwezi January mwaka huu 2012.

Arist Nick name: C-SIR MADINI (Sisa)
Real Name: PETER MPONEJA
Birthdate: 07th may 1992
New release: PAIN KILLER
Written by: Kid bwoy
Produced by: Kid bwoy
Studio: Tetemesha Records


“PAIN KILLER” Lyrics by C-SIR MADINI (SISA)
Written by: Kid bwoy
Produced by: Kid bwoy
Tetemesha Records, 2012

Intro:
We ndo ma painkiller
Ooh ma ma ma ma, oooh
Tam tam oooh, yako tam tam
Tam tam oooh, yako tam tam

Verse 1:
Mwanzo aliniona kwenye twitter, kabla jina sijalipata,
Kifungo huru ilimvuta, nishike mkono ikafata,
Ana sifa nyingi kaumbika, sauti ka mtoto amepita,
Top ten yama miss wa bongo, namba moja ashaipata,

Bridge :
Nikikatiza nae kitaa watu wote ndalile, oooh wanabaki ooooh,
Usijaribu fata hii asali yangu ndalile, oooh utalia oooooh,x 2

Chorus:
Ye ndo pain killer yangu, moyo hauna utata,
Yeye ndo tekila yangu, siogopi ukata,
Ye ndo medulla yangu, stress zikinikamata,
Ye ndo cellular yangu, nilipo utamkutaaa,
Aiyaa taiyaaaa, aaaaaaaah x2

Verse 2:
Kama ni nguo ye si mtumba kipya kinyemi wadananda ndo mjue, hai
Tena nitafuga mbwa nshaweka fensi wadoezi msinijue, hai
Kama ni nguo ye si mtumba kipya kinyemi wadananda ndo mjue,
Tena nitafuga mbwa nshaweka fensi wadoezi msinijue,
Una create attention, attention lazima watupishe, hai
Unawaongezea tention, tension lazima watupishe, hai
Una create attention, attention lazima watupishe,
Unawaongezea tention, tension lazima watupishe,
Bridge :
Nikikatiza nae kitaa watu wote ndalile, oooh wanabaki ooooh,
Usijaribu fata hii asali yangu ndalile, oooh utalia oooooh,x 2

Chorus:
Ye ndo pain killer yangu, moyo hauna utata,
Yeye ndo tekila yangu, siogopi ukata,
Ye ndo medulla yangu, stress zikinikamata,
Ye ndo cellular yangu, nilipo utamkutaaa,
Aiyaa taiyaaaa, aaaaaaaah x2

Verse 3:
We ndo ma pain killer, aaaaaaah
We ndo ma heart desire, aaaaaaaah

Pilipili pili yako tam tam ooooh, yako tam tam
pili pili yako tam tam ooooh, yako tam tam
Nyanya chungu yako tam tam ooooh, yako tam tam
Nyanya chungu yako tam tam ooooh, yako tam tam x2

Chorus:
Ye ndo pain killer yangu, moyo hauna utata,
Yeye ndo tekila yangu, siogopi ukata,
Ye ndo medulla yangu, stress zikinikamata,
Ye ndo cellular yangu, nilipo utamkutaaa,
Aiyaa taiyaaaa, aaaaaaaah x2

Outro:
Tam tam oooh, C-sir Madini
Tam tam oooh, Tetemesha
Tam tam ooh, yako tam tam
Da nda da da nda da danda da da nda da
Da nda da da nda da danda da da nda da, uuh
Da nda da da nda da danda da da nda da, uuh
Da nda da da nda da danda da da nda da...
Aaaaaaaah aaaaaaah aaaaaaah
END  

MKUU WA MKOA WA MBEYA ABAS KANDOLO AMEVUNJA BARAZA LA MADIWANI WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA NA KUTANGANZA RASMI HALMASHAURI YA RUNGWE ITAKAYO KUWA NA KATA 26 NA KUITANGAZA HALMASHAURI YA BUSOKELO ITAKAYOKUWA NA KATA KUMI NA MOJA.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbass Kandolo 
Mkuu wa mkoa wa mbeya Abass kandolo amevunja baraza la madiwani wilaya ya rungwe mkoa wa mbeya na kutanganza rasmi halmashauri ya rungwe itakayo kuwa na kata 26 na kuitangaza halmashauri ya busokelo itakayokuwa na kata kumi na moja.
Akiongea na baraza la madiwani mkuu wa mkoa wa mbeya amsema kuwa serikali imeanzisha kifungu (sub_vote) na>7813140 na kutenga fedha kwenye bajet ya mwaka wa fedha 2012/2013 kwa ajili ya halmashauri ya busokelo, yenye jumla ya tsh 12,549,250,889/=
Halmashauri ya rungwe itakuwa ikiongozwa na mkurugenzi noel mahyenga pia halmashauri ya busokelo itakuwa inaongozwa na imelda ishuza aliyeteuliwa kuiongoza halmashauri ya busokelo inayoanza leo kuwahudumia wananchi wa busokelo.
Akitoa saram za mkoa mkuu wa mkoa wa mbeya kandolo amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii na kuchangia shughuri za maendeleo na hili itazizifanya halmashauri kuwa maendeleo zaidi.
Pia amesema haitakuwa na maana kuwa na halmasahauri mbili bila ya kujibidisha kufanya kazi za maendeleo na kukusanya ushuru ili kujiwezesha kujitegemea
Zaidi amewapongeza wananchi wa busokelo kupata huduma za maendeleo karibu na wao
Amewahakikishia kuwa serikali kwa kuzingatia ahadi ya rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania dr jakaya kikwete aliyoitoa katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ombi lililotolewa na mbunge wa rungwe masharika prof mark mwandosya katika kiwanja cha tandale na rais aliahidi kuifanya wilaya ya rungwe kuwa na halmashauri mbili rungwe na busokelo na leo ahadi hiyo imetimia kwa kupata halmashauri ya mpya ya busokelo.

Baraza la Madiwani kabla ya kuvunjwa

MKUU WA WILAYA RUNGWE CYPRIAN MEELA AKIONGEA NA MADIWANI

KABLA BARAZA LA MADIWANI HALIJAVUNJWA

Wednesday, October 10, 2012


SERIKALl inaonekana haitaki tena mchezo katika taasisi zake na hivyo imeamua kuchukua uamuzi mzito kwa kuendelea kusimamisha kazi wakuu wa taasisi hizo ili kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali. Hatua hizo zinalenga kuondoa malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na wananchi dhidi ya utendaji mbovu wa baadhi ya viongozi hao, lakini pia ikitafuta kujiridhisha kwa kuthibitisha tuhuma hizo kwa ushahidi usio na shaka. Lengo pia ni kuhakikisha kila mtu anatendewa haki na hakuna anayeonewa na hatimaye utendaji kazi serikalini na katika taasisi zake unakuwa wa kuridhisha. Wimbi la viongozi hao kusimamishwa liliendelea jana, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Joseph Mgaya alisimamishwa kazi kwa tuhuma za ununuzi wa dawa bandia za kupunguza makali ya Ukimwi (ARV). Mbali na Mgaya, wengine waliosimamishwa pamoja naye ni Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora, Sadiki Materu na Ofisa Udhibiti wa Ubora, David Masero. Mgaya anakuwa kiongozi wa sita wa taasisi nyeti nchini kusimamishwa kazi kwa tuhuma hizo kwa mwaka huu. Serikali pia kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), imesitisha uzalishaji wa dawa zote katika kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Limited (TPI) hadi uchunguzi unaofanywa kupitia vyombo vya usalama kuhusu uzalishaji wa dawa bandia utakapokamilika kwa hatua zaidi za kisheria. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi alisema tuhuma za MSD kununua dawa bandia kutoka TPI ziligundulika baada ya matokeo ya ukaguzi, ufuatiliaji na uchunguzi wa kimaabara. Alisema mwanzoni mwa Agosti, Wizara kupitia TFDA kwa kuzingatia Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi ilibaini kuwapo ARVs bandia aina ya TT-VR 30 toleo namba OC.01.85 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara. Baada ya kubainika kwa tatizo hilo, Dk Mwinyi alisema Wizara kupitia TFDA ilifanya ukaguzi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya katika Mkoa wa Mara na baadaye ukaguzi wa kina katika mikoa mingine nchi nzima kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama. “Ukaguzi huu ulifanyika kati ya Agosti 6-31 mwaka huu na ulihusisha MSD makao makuu na kanda pamoja na kiwanda cha TPI ambacho ndicho kilitengeneza dawa hiyo. Pia sampuli za dawa husika zilichukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara,” alisema. Alisema baada ya kubaini tatizo hilo, waliwataarifu waganga wakuu wa mikoa yote nchini na kuwaelekeza wasimamishe matumizi ya ARVs toleo namba OC.01.85 katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya katika mikoa yao. Mbali na kusitisha matumizi, waganga hao walielekezwa kuiondoa dawa hiyo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na kuirudisha kwa msambazaji ambaye ni MSD na Wizara kupitia TFDA ilifanya uchunguzi wa kimaabara ili kuainisha viambata vya dawa hiyo. Dk Mwinyi alisema katika ukaguzi na ufuatiliaji huo pamoja na uchunguzi wa kimaabara, walibaini kwamba dawa yenye jina la biashara TT-VIR 30 toleo namba OC.01.85 ni bandia kwa mujibu wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi . “Nyaraka zilizopo zinaonesha kuwa kiwanda cha TPI waliiuzia MSD dawa hiyo bandia na ilitengenezwa Machi mwaka jana na muda wake wa matumizi unakwisha Februari 2013,” alisema Dk Mwinyi. Kwa mujibu wa Dk Mwinyi, dawa hiyo bandia ilikuwa na rangi mbili tofauti ambazo ni njano na nyeupe; zilizokuwa na rangi ya njano zilikuwa na kiambata cha Efaverenz badala ya viambata aina ya Niverapine, Lamivudine na Stavudine vilivyopaswa kuwepo. “Vidonge vyenye rangi nyeupe vilikuwa na viambata vinavyotakiwa kuwepo yaani Niverapine. Vidonge vilivyokutwa kwenye vifungashio vya dawa husika vilikutwa tofauti na vifungashio vilivyosajiliwa na TFDA,” alisema. Hatua mbadala Dk Mwinyi alisema Wizara itahakikisha kuwa ARVs zipo za kutosha na zenye ubora unaotakiwa na zitaendelea kupatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya kote nchini. Aliwakumbusha waganga wakuu wa wilaya na mikoa kuimarisha kamati za dawa na tiba katika vituo vya huduma za afya, ambazo zina majukumu ya kusimamia upokeaji, uhakiki wa ubora na matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba. Pia alisema matarajio ya wizara ni kuendelea kuimarisha mfumo na taratibu za uhakiki wa ubora, utunzaji, usambazaji na matumizi ya dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini. Alitoa rai kwa jamii kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa pale wanapobaini kuwapo dawa zenye ubora wenye shaka au uvunjifu wa sheria inayosimamia ubora na usalama wa dawa. Alihimiza wananchi kuendelea kutumia ARVs kwa kuwa dawa hiyo yenye shaka imekwishaondolewa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Hata hivyo, waandishi walipotaka kufahamu endapo kuna wananchi waliojitokeza kutokana na athari za dawa hizo, Dk Mwinyi alisema mpaka sasa hajapokea ripoti yoyote na uchunguzi umefikia katika hali nzuri na hivi karibuni utakamilika. Pia alisema mpaka sasa wamerudisha makopo 9,570 ya dawa hizo bandia na makopo 2,600 yanaendelea kukusanywa na kurudishwa. Waliosimamishwa kabla Mei 18, Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda alimsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege ili kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma zinazomkabili ikiwamo ya kampuni hewa za ukaguzi wa magari nje ya nchi. Juni 5, aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) Paul Chizi alisimamishwa kazi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kutokana na ukiukwaji wa sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2003 kifungu 17(1) au (3). Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando, alisimamishwa kazi Julai 14 kupisha uchunguzi juu ya tuhuma dhidi yake za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka. Julai 19, Bodi ya Wakurugenzi wa benki ya NBC ilimlazimisha Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo, Lawrence Mafuru kwenda likizo ili kupisha uchunguzi juu ya ubadhirifu. Hata hivyo baada ya uchunguzi, Mafuru hivi karibuni alirejeshwa kazini baada ya Bodi kuridhika kuwa hakufanya ubadhirifu wowote. Agosti 23, Waziri wa Uchukuzi Dk Mwakyembe alimsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Ephrahim Mgawe na wasaidizi wake wawili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

BREAKING NEWS:- Soko la UYOLE MBEYA Linateketea kwa moto


BREAKING NEWS:- Soko la UYOLE MBEYA Linateketea kwa moto Soko la Uyole mkoani Mbeya linateketea kwa moto, jitahada za kuuzima zinaendelea, chanzo cha moto huo bado hakijajulikana

Tuesday, October 9, 2012

Mume ajinyonga kwa kunyimwa unyumba

MKAZI wa Mtaa wa Mpanda Hotel wilayani Mpanda katika Mkoa wa Katavi, Nzego Vicent (33) amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya katani huku akimlalamikia mkewe kwa kumnyima unyumba kwa siku tatu mfululizo bila kupewa sababu zilizomridhisha.

Mashuhuda wakiwemo baadhi ya majirani wa wandoa hao kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini, walidai kabla ya kujinyonga, Vicent ambaye alikuwa ametoka kunywa pombe za kienyeji, alifika nyumbani kwake saa 6:20 usiku na kumtaka mkewe ampe unyumba.

Majirani hao walidai kuwa mke wa marehemu, Agnes Nicodemu alilalamikia mumewe kuwa hakuwa tayari kumpatia unyumba kutokana na shughuli alizokuwa amezifanya mchana kutwa na kumsihi avumilie hadi siku itakayofuata kwa kuwa alikuwa amechoka sana.

“Siku mbili mfululizo mama huyo kutokana na kuelemewa na kazi nzito za shamba na nyumbani kwake ambazo alikuwa akizifanya kuanzia alfajiri hadi usiku wa manane, aliendelea kumsihi mumewe ambaye alikuwa akirudi nyumbani usiku kuwa amechoka,“ alidai mama mmoja jirani na wanandoa hao.

Inadaiwa kuwa baada ya Vicent kujibiwa hivyo kwa siku tatu mfululizo hakuridhika na madai hayo ya mkewe ndipo alipoanza kumshutumu kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na wanaume wengine.

Inadaiwa siku ya tatu, Vicent alimshambulia mkewe huyo kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake huku akimtolea maneno ya kumtisha kuwa lazima atamuua kwa mapanga iwapo ataendelea kuwa mkaidi katika unyumba.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, baada ya kuona kipigo kimezidi mwanamke huyo alikimbia nje ili kukwepa kipigo na mumewe naye alitoka nje ya nyumba yao akiwa ameshikilia mashoka mawili na kwenda kusikojuliakana na kuiacha nyumba ikiwa wazi.

Ilipotimu saa 12:30 alfajiri, mwanamke huyo alifuatwa na majirani waliomweleza kuwa mumewe amejinyonga kwa katani jirani na nyumba waliyokuwa wakiishi ndipo alipoandamana nao hadi eneo hilo na kumuona akiwa amening’inia juu ya mti.
MKAZI wa Mtaa wa Mpanda Hotel wilayani Mpanda katika Mkoa wa Katavi, Nzego Vicent (33) amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya katani huku akimlalamikia mkewe kwa kumnyima unyumba kwa siku tatu mfululizo bila kupewa sababu zilizomridhisha.

Mashuhuda wakiwemo baadhi ya majirani wa wandoa hao kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini, walidai kabla ya kujinyonga, Vicent ambaye alikuwa ametoka kunywa pombe za kienyeji, alifika nyumbani kwake saa 6:20 usiku na kumtaka mkewe ampe unyumba.

Majirani hao walidai kuwa mke wa marehemu, Agnes Nicodemu alilalamikia mumewe kuwa hakuwa tayari kumpatia unyumba kutokana na shughuli alizokuwa amezifanya mchana kutwa na kumsihi avumilie hadi siku itakayofuata kwa kuwa alikuwa amechoka sana.

“Siku mbili mfululizo mama huyo kutokana na kuelemewa na kazi nzito za shamba na nyumbani kwake ambazo alikuwa akizifanya kuanzia alfajiri hadi usiku wa manane, aliendelea kumsihi mumewe ambaye alikuwa akirudi nyumbani usiku kuwa amechoka,“ alidai mama mmoja jirani na wanandoa hao.

Inadaiwa kuwa baada ya Vicent kujibiwa hivyo kwa siku tatu mfululizo hakuridhika na madai hayo ya mkewe ndipo alipoanza kumshutumu kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na wanaume wengine.

Inadaiwa siku ya tatu, Vicent alimshambulia mkewe huyo kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake huku akimtolea maneno ya kumtisha kuwa lazima atamuua kwa mapanga iwapo ataendelea kuwa mkaidi katika unyumba.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, baada ya kuona kipigo kimezidi mwanamke huyo alikimbia nje ili kukwepa kipigo na mumewe naye alitoka nje ya nyumba yao akiwa ameshikilia mashoka mawili na kwenda kusikojuliakana na kuiacha nyumba ikiwa wazi.

Ilipotimu saa 12:30 alfajiri, mwanamke huyo alifuatwa na majirani waliomweleza kuwa mumewe amejinyonga kwa katani jirani na nyumba waliyokuwa wakiishi ndipo alipoandamana nao hadi eneo hilo na kumuona akiwa amening’inia juu ya mti.